• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Serikali kutowavumilia watakao vamia Msitu wa Mkoa Singida

Posted on: May 11th, 2023

Serikali ya Mkoa wa Singida imesema haitamvumilia mtu yeyote atakayefanya shughuli za kilimo, ufugaji au ujenzi kwenye hifadhi ya msitu wa Mkola uliopo kata ya Mgori Wilaya ya Singida vijijini kwa kuwa uharibifu uliofanyika eneo hilo una athari endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba leo wakati alipotembelea eneo la msitu  kwa lengo la kujionea uharibifu uliofanywa na wananchi ambao wamekata miti na kufungua mashamba huku wengine wakianzisha makazi na kufanya shughuli za ufugaji katika msitu huo.

Akiongea na wananchi hao wa Kijiji cha Mkola na Msikii ambao ndio  wamiliki wa  msitu huo RC Serukamba aliamuru kukamatwa kwa watu watano  wakiume wakiwa wanne na mwanamke mmoja ambao walifyeka miti inayokadiriwa kufikia 8,000 iliyopandwa na Serikali mwaka jana na wakafungua mashamba ambapo yamelimwa alizeti kwa sasa.

Akiwa katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho alitaja majina ya wakulima waliovamia msitu huo na  kutoa vitisho kwa viongozi wa Kijiji wakidai kwamba hawana maeneo mengine ya kuendesha shughuli zao.

Watuhumiwa hao watano kati ya wanane walikamatwa na Jeshi la Polisi huku wengine wakiendelea kusakwa ili wafikishwe Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo Mtendaji wa Kijiji  na Mwenyekiti wa Kijiji cha Msikii wametakiwa tarehe 12.5.2023 kufikisha majina ya watu wote wanaolima katika maeneo hayo kwakuwa ndio wanao tuhumiwa kukaidi amri ya Serikali.

RC aliwataka Serikali za vijiji kutumia Sheria na taratibu kuhakikisha msitu huo unalindwa kwa  gharama yeyote bila kumuonea mtu kwa kuwa  kulima maeneo ya mlimani kumesababisha watu wengi upande wa Kijiji cha Mkola kupoteza makazi yao kwa kupata mafuriko.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragili amesema msitu huo wenye hekta 1393.6 una umuhimu mkubwa katika utunzaji wa mazingira na Vijiji hivyo viliwahi kutoa Milioni 17 kwa ajili ya utunzaji wa msitu huo hivyo lazima utunzwe.

Alisema mwaka juzi walishirikiana na Vijiji hivyo wakapanda miti 6,000 na mwakajana wakapanda tena miti 8,000 lakini inashangaza kuona miti imekatwa yote na mingine imeliwa na mifungo jambo ambalo amesema Serikali haitalifumbia macho.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.