• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERIKALI KUWAUNGANISHA WAZALISHAJI WAKUBWA WA CHAKULA KATIKA KATA TANO WILAYANI IRAMBA..

Posted on: July 2nd, 2017

  Serikali imedhamiria kuwaunganisha wakulima wakubwa wa mazao ya chakula wa kata tano za Wilaya ya Iramba kwa kujenga daraja na makaravati manne katika barabara yenye urefu wa kilomita 38.6 yatakayo gharimu shilingi bilioni 4.1.

Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Mto Mtoa na makaravati katika barabara ya shelui-Mtoa-Urughu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour amesema serikali imedhamiria kuwaunganisha wananchi ili wazalishe mazao, waanzishe viwanda kisha kusafirisha bidhaa.

Amour amesema kwakuwa barabara hiyo inahudumia wananchi wa  kata za Shelui, Mtoa, Mtekente, Urughu na Ndago wananchi wa maeneo hayo watumie fursa ya kuwa na barabara nzuri kwa kutengeneza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa na kisha kusafirisha bidhaa na sio mazao kama mali ghafi.

Amesema kwa kufanya hivyo wakulima wa mazao wataweza kujiongeza kipato chao kwa kuwa hawatapunjwa kwa kuuzwa mali ghafi ambayo hupelekwa kwenye viwanda vya nchi nyingine hivyo barabara hiyo iwe hamasa kwao kuzalisha kwa wingi pamoja na kuanzisha viwanda  kwa wingi.

Mradi huo wa barabara na makaravati unatekelezwa kupitia mpango wa kuondoa vikwazo kwenye barabara za vijijini, mpango unaofadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kushirkiana na serikali za Uingereza na Ireland Kaskazini.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja na makaravati hayo kutawezesha barabara hiyo kupitika kwa kipindi cha mwaka mzima na hivyo kuwanufaisha wakazi elfu 79 wa kata hizo pamoja na kuwezesha utoaji wa huduma za kijamii katika eneo hilo lenye shule za msingi 29, shule za sekondari 6, zahanati 7 na kituo cha afya kimoja.

Wakati huo huo Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour amezindua mradi wa ghala la kuhifadhia chakula katika kijiji cha Nselembwe ambalo litakuwa likihudumia jamii ya kata za Ulemo,Mgongo, Ntwike, Shelui na Mtoa.

Akifungua ghala hilo Amour amesema kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya taifa hivyo ujenzi wa ghala ili kuhifadhi mazao unasaidia wananchi kutoyauza ovyo mazao na kuyahifadhi mahali salama kabla ya kuyachakata kuwa bidhaa.

Amesema mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 350 utaweza kuwasaidia wananchi kuhifadhi mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwa na kauli moja juu ya bei ya mazao pia watakua na uhakika wa mazao.

Amour amewasisitiza wananchi wa kata hizo kuzalisha kwa wingi kwa kuwa sasa wana uhakika wa sehemu salama ya kutunzia mazao yao ili wasishawishike kuyauza kwa bei ndogo.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Iramba umetembelea miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 huku ukipitia miradi 6 na kuona shughuli 5 katika vijiji  10 na tarafa 4 katika umbali wa km 119.1.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.