• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERIKALI MKOANI SINGIDA, IMEAGIZA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU NA KUCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 WAHAKIKISHE WANARIPOTI KWA WAKATI KATIKA SHULE ZAO WALIZOPANGIWA HATA KAMA HAWANA SARE ZA SHULE.

Posted on: January 10th, 2019

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, amesema cha kuzingatia zaidi ni mwanafunzi awe na madaftari na kalamu.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya meza na viti kwa shule za Sekondari kutoka halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2019. Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya kata ya Ikungi.

Amesema kuwa, haamini kama kuna mzazi au mlezi yeyote atakayeshindwa kumudu kununua sare ya mtoto wake. Amedai kuwa, kwa mkoa wa Singida unavyosifika kwa ufugaji wa kuku mzazi au mlezi akiuza kuku watatu tu wa kienyeji (akiwaita kuku wa Singida), atanunua sare na kubakiwa na chenji.

“Mtoto (mwanafunzi) atakayekosa sare, basi nguo atakazoenda nazo shule ziwe na hadhi ya shule (nguo zenye maadili ya shule), zisiwe zile ambazo zitamkosesha amani mtoto. Zikiwa choka mbaya, zitamchanganya kisaikolojia mwanafunzi na hivyo hatofanya vizuri kwenye masomo yake”, Amesema Dkt. Nchimbi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi, amesema kuwa, wanatarajia kutumia zaidi ya shilingi 29.9 milioni, kwaajili ya kugharamia utengenezaji wa meza 700 na viti 700.

Alisema fedha hizo zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na pia kutoka kwenye Mfuko wa Jimbo.

Kijazi amesema lengo la kutengeneza meza na viti hivyo ni wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu (2019), wanaingia madarasani.

Akisisitiza zaidi, mkurugenzi mtendaji huyo amesema, utengenezaji wa meza na viti hivyo ni mikakati waliojiwekea kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ndani ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi wajiunge na shule walizochaguliwa bila kuwa na vikwazo.

Bw. Kijazi ameeleza kuwa, jumla ya wanafunzi 1,572 wamemaliza kidato cha nne mwaka jana, na wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 4,690.

“Kuna ongezeko la wanafunzi 2,118. Ongezeko hili la wanafunzi limepelekea upungufu wa vyumba vya madarasa 23 vitakavyokidhi wanafunzi 376. Ongezeko hilo vile vile limesababisha upungufu wa viti 2,118 na meza 2,118”, Kijazi alifafanua zaidi.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Bw. Kijazi amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kutumia mapato ya ndani pamoja na fedha za Mfuko wa Jimbo la Magharibi inatengeneza jumla ya viti 700 na meza 700.

Hivyo katika awamu hii ya kwanza, Halmashauri imetengeneza viti 600 na meza 600 kwa kutumia mbao 542 zilizopatikana msituni kwa wavunaji haramu, mbao za kununua pamoja na fedha taslimu kutoka mapato ya ndani shilingi 19,935,000/= na fedha za mfuko wa jimbo la Magharibi shilingi 10,000,000/=, hivyo kufanya jumla ya fedha zote ni shilingi 29,935,000/=. Kwa sasa halmashauri ya wilaya imeanza kukamilisha meza 100 na viti 100 ili kukamilisha utengenezaji wa meza 700 na viti 700.

Aidha, Kijazi amesema kila Kata inaendelea kutengeneza meza na viti kwa mujibu wa mahitaji ya shule zilizopo katika Kata hizo. Hadi sasa jumla ya meza 497 na viti 636 zimekwishatengenezwa.

“Hivyo, kila Mtoto (mwanafunzi) aliyefaulu kujiunga na masomo ya Sekondari 2019 atakuwa ameenda shule ambako atakuta KITI na MEZA na hivyo kusoma bila ya kikwazo chochote. Ni matarajio yetu kuwa kwa shule ambako bado kuna changamoto chache zilizobaki watakamilishiwa kwa muda mfupi” Amesema Bw. Kijazi.

Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, alisema ofisi yake inafuatilia kwa karibu sekta ya elimu na hasa kipindi hiki shule zinapofunguliwa.

.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.