• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Serikali yadhamiria kuwaondoa wavamizi wa Msitu wa Mgori Wilayani Singida

Posted on: July 13th, 2022


Serikali imedhamiria kuwaondoa wavamizi wa Hifadhi ya msitu wa Mgori wenye ukubwa wa kilomita za mraba elifu 49 ambao umevamiwa na wnanchi kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi kilimo uvufugaji na uchomaji wa mkaa hivyo kusababisha  uharibifu mkubwa  wa mazingira.

Akiongea wakati wa ziara yake iliyofanyika hivi karibuni  katika hifadhi ya msitu huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge akiwataka wananchi wote waliovamia kuondoka wenyewe huku akiwataka wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na kamanda wa polisi Mkoa wa singida Kuhafanya doria na kuwakamata wote watakao kaidi agizo hilo.

RC Mahenge amesema, uharibifu wa msitu huo umeongezeka  ikilinganishwa na mwaka jana ambapo alijioea alipotembelea eneo hilo na kutoa maagizo ya kutolewa kwa elimu ili wavamizi waweze kuondoka wenyewe lakini bado hali imeendelea kuwa mbaya baada ya wengine kuja na kuanzisha makazi  eneo hilo.

“Si mara ya kwanza kutembelea msitu huu leo ni mara ya pili lakini naona uharibifu umeendelea kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka jana natoa maelekezo mengine kwa wakala wa huduma ya misitu Tanzania na TFS kwa kushirikiana na kamamnda wa polis mkoa kufanya doria katika eneo hili kila wiki mara moja na na nitafanya mawasiliano na wiazara ya maliasili na utalii ili kuona namna ambavyo wanaweza kuingiza msitu huu kwenye hifadhi zaio.” Alisema RC Mahenge.

 Aidha amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasikas Muragili kuhakikisha ulinzi shirikishi unakuwepo kwa kuwashirikisha wananchi na viongozi wa vijiji vinazunguka msitu  ikiwa na pamoja na kuandaa mkakati wa muda mrefu wa namna ya kulinda msitu huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya  hiyo Mhandisi Pasikasi Muragili amemueleza mkuu wa mkoa huo kwamba walitoa elimu katika  vijiji vyote vinavyoizunguka hifadhi hiyo ikiwemo kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi ambao walionekana kushiriki kuwaingiza waavamizia ndani ya msitu ambapo kesi zao bado zinaendelea.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida  Vijijini Elia Digha  akaiomba serikali kutilia mkazio ulizi wa msitu huo ambao kwa mkoa wa singida umebaki mmoja TU,huku akieleza kwamba tayari  wapo wananchi ambao wamevamia katika kijiji cha Muhunga kata ya Mgori wilaya ya singida.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba zoezi la kuwandoa wavamizi hao limefanika Zaidi ya mara moja lakini inaonekana kuja wengine wapya jambo ambalo linahitaji ushirikiano baina ya serikali ili kulimaliza kabisa.

Hata havyo amesesisitiza kwamba wapo wananchi waliha ondolewa ambao bado wanasubuiria serikali kuwapatia eneo jingine la makazi na kilimo jambao ambalo Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba serikali inaweza kulifikiria na kulitolewa majawabui ili wananchi hao waweze kufahamu kinachoendelea.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya  Mughunga , Nassoro Hassan  amesema uvamizi wa msitu unasababishwa na ulizni mdogo ambapo doria ya mara kwa mara imeonekana kwuwa muoarobaini wa changamooto hiyo.

 Amesema wananchi wa kijiji chake wapo tayari endepo watapatiwa polisi hata  wawili kushiri kikamilifu kuwaondoa waavamizi hao kwa kuwa wamekuwa ni hatari hata kwa maisha yao kutokana na  wavamizi hao kutumia silaha za jadi kama upinde na mishale kupambana na watu wanaowazuia kuingia katika msitu huo.

Awali akitoa taarifa yake  kwa Mkuu wa Mkoa Muhifadhi wa Misitu wa Wilaya ya Singida, Uswege Mwasumbi  amesema tokea maagizo ya serikali ya kulinda msitu huo mwaka jana kutolewa wamchoma vibanda 704 vilivyokuwa vimejengwa kwenye hifadhi na kuwaondoa watu kwenye makazi hayo lakini inaonekana bado wanarudi au kuja wengine.

Amesema maelekezo yaliyotolewa na viongozi hao watayatekeleza ikiwemo ya kufanya doria ya mara kwa mara pamoja na kuchoma moto vibanda vitakavyojengwa na kuwafungulia mahstaka wote watakokuwa wamekamatwa katika msitu huo.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mughunga  wameiomba serikali kuwapatia maeneo ya kulima na kujenga nyumba kwa kuwa wameondolewa katika eneo la hifadhi ambalo walingia kwa kutojua kama ni eneo la msitu jambo ambalo lilitolewa ufafanuzi na mkuu wa wailaya hiyo Mhandisi Pasikasi Muragili kwamba tayari wananendelea na utaratibu wa upimaji ili kuweza kuyatenganisha mazeneo ya makazi na  higfadhai

Hata hivyo RC Mahenge alitawataka waanchi hao waliokubali kuondoka katika eneo la msitu kuendelea na utulivu walionao wakati serikali ikiangalia  namna ya kuwapatia maeneo mengine mbadala.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.