• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERIKALI YAPATA ‘MWAROBAINI’ KUKABILI CHANGAMOTO ZA WASANII WA FILAMU NCHINI

Posted on: January 23rd, 2020

HATIMAYE Serikali imepata majawabu yatakayosaidia kupunguza changamoto sugu za wasanii nchini, ikiwemo tatizo la muda mrefu la ‘ukata’ wa maisha na mitaji duni katika kuwawezesha kuzalisha kazi zao kwa viwango na ubora stahiki kulingana na mahitaji ya soko

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa filamu, mkoani hapa jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dk Kiagho Kilonzo, alisema kasi ya mafunzo ya muda mfupi yaani ‘masterclases’ inaendelea katika kuwawezesha wasanii wa tasnia hiyo kuboresha kazi zao

“Mpaka sasa mafunzo yamefanyika kwenye mikoa tisa nchini chini ya ufadhili wa serikali, ya namna ya kuboresha uzalishaji wa filamu kupitia mafunzo ya muda mfupi,” alisema Kilonzo

Aidha, alisema juhudi za serikali za kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kwa lengo la kutafuta wataalamu mbalimbali wa kuendesha programu za mafunzo zimeendelea kutoa matumaini, ambapo mpaka sasa tayari wamefanikiwa kuwapata, na muda wowote wasanii watatangaziwa utaratibu wa mafunzo hayo ili kupata fursa ya kushiriki

Kilonzo ambaye alikuwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuzungumza, alisema juhudi zilizopo kwa sasa wanaendelea kutafuta soko la uhakika la filamu za kitanzania ili kuwapa wazalishaji na wadau wote hamasa ya kufaidi matunda ya kazi zao

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk Kiagho Kilonzo akizungumza kwenye kikao hicho.

“Mpaka hivi ninavyozungumza tayari wanigeria wamejitokeza wanahitaji hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu wawe na ‘story’ kati ya hamsini hadi mia moja za kitanzania, hivyo nawahimiza wasanii changamkieni fursa hiyo anzeni kutengeneza hadithi za kiafrika zinazoweza kuuzika nje ya Tanzania,” alisema

Mbali na hilo, wadau wa filamu kutoka taifa la Namibia nao pia wameonyesha utayari wa kufanya ‘uzalishi shirikishi’ kwa kuungana pamoja na wasanii wa filamu wa kitanzania kutengeneza kazi zitakazouzwa nchi zote mbili, taarifa kamili kuhusu mchakato huo unatarajiwa kutangazwa kuanzia mapema mwezi Machi mwaka huu

Aidha, Kilonzo alisema ili kuboresha kipato na kukabiliana na changamoto ya ajira kwenye tasnia ya filamu nchini, Serikali ikiwa ndani ya taifa la Uingereza, ilikutana na makampuni 15 ambayo yalionyesha nia ya kuja kuwekeza nchini, na yatakapowasili kulingana na kanuni na taratibu za Tanzania basi wawekezaji hao wa filamu watalazimika kuchukua sehemu kubwa ya nguvu kazi ya ndani ya watanzania

Sambamba na hilo, alisema wadau wa Shirikisho la Filamu kutoka India ‘Bollywood’ nao mapema mwezi Juni watawasili nchini, ambao tayari wamehitaji kupata wasanii wa kitanzania wapatao 100, ili kushirikiana kwa pamoja katika kukamilisha azma yao

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (wa tatu kulia) akisikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wadau wa filamu mkoani singida jana, wa kwanza kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Singida, Henry Kapella, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dk Kiagho Kilonzo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida, Wilson Shimo.

Hata hivyo, mchakato wa Bodi uliopo kwa kushirikiana na wadau, ni kuanza kushindanisha kazi mbalimbali za Sanaa ya Filamu kupitia kumbi za maonyesho lengo likiwa ni kupata filamu moja bora ambayo hatimaye itaingia kwenye soko la kimataifa, na sehemu ya fedha ya viingilio atapewa mzalishaji wa kazi husika

Akizungumzia kuhusu hatua ya upatikanaji wa Katiba ya Shirikisho unaoendelea, Kilonzo alisema serikali imeweza kudhamini kikamilifu hatua kwa hatua mchakato huo kwa mafanikio, huku hatua iliyobaki kwa sasa ni ile ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho ambao unatarajiwa kukaa kwa mara ya mwisho ifikapo Januari 28 mwaka huu

“Hatua zilizofikiwa mpaka sasa ni kwamba Serikali iliunda timu kupitia ile Katiba na kuizungusha nchi nzima, na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari ili kutoa fursa ya wadau kutoa maoni yao kutaka iweje, na mpaka sasa mkutano mkuu umeshakaa vikao viwili huku kile cha mwisho kikisubiriwa,” alisema

Kwa upande wake, Shonza pamoja na mambo mengine, aliwataka wasanii wa filamu nchini kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, ili kwenda sanjari na mahitaji ya walaji kwa kuzingatia vigezo vyote muhimu, huku akirudia kusisitiza suala la ubora mara kwa mara

Alisema barani Afrika Tanzania inashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa filamu nyingi, ikitanguliwa na Nigeria, huku akiwataka wasanii kujipanga kwanza na hatimaye kutoa angalau filamu moja tu kwa mwaka itakayokuwa na ubora na hatimaye kuweza kumtambulisha vizuri zaidi msanii kwenye soko

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizungumza na Wadau wa Filamu mkoa wa Singida jana.


Shonza aliwataka wasanii kote nchini kuondokana na mfumo wa kutengeneza movie na kuweka kwenye DVD huku akisema ni rahisi kuibiwa, badala yake msanii aanze kwanza kwa uzinduzi kwenye kumbi za sinema kabla ya kutupia kwenye mtandao ili msanii kujihakikishia idadi kubwa ya watazamaji na soko la uhakika

“Nataka niwakikishie kuwa filamu za watanzania zinapendwa sana, na wala tatizo sio masoko…soko lenyewe la Afrika Mashariki bado hatujalimaliza, kinachotakiwa kwa sasa ni kuboresha filamu zetu ziwe katika ubora,” alisema na kuongeza:

“Kama tatizo ni fedha jiongezeni jiungeni kwenye vikundi, nendeni Halmashauri kuna mikopo ya vijana, wanawake na wenye ulemavu, ipo kisheria pale asilimia 10 imetengwa, kachukueni mfanye ujasiriamali na faida mtakayoipata boresheni sanaa yenu”.

Wasanii na wadau mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani).

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.