Serikali imetoa power benk 200 katika maeneo ambayo yanachangamoto ya ukosefu wa umeme Mkoani Singida kama sehemu ya utatuzi wa changamoto ya kuishiwa chaji kwa vishikwambi ambavyo vinatumiwa na Makarani wa Sensa ya watu na Makazi ya 2022.
Akiongea baada ya kuwatembelea Makarani hao katika Manispaa ya Singida, Singida Dc na Wilaya ya Mkalama Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema Serikali imetoa Power Benk hizo kwa kuwa jana uzoefu umeonesha baadhi ya maeneo Makarani kupata changamoto baada ya vitendea kazi vyao kumaliza chaji kabla ya muda.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akizungumza na Karani wa Sensa wakati wa ziara yake Singida Vijijini
Amesema kutokana na ukaguzi alioufanya kupitia Makarani wapata Tisa ameona zoezi linaendelea vizuri na kuna kila dalili ya kumaliza zoezi hilo ndani ya muda na kila mwananchi kufikiwa.
RC Serukamba amawaomba wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano mkubwa kwa Makarani ikiwemo kuwaruhusu kuchaji vishikwambi vyao kwenye makazi yao wakati wakiendelea kuhesabu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili amesema zoezi linaendela vizuri na haijatokea changamoto yoyote kwa kuwa wataalamu wa tehema wamekuwa karibu na Makarani kwa ajili ya utatuzi wa changamoto yoyote itakayojitokeza.
Aidha amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kwa upande wa Wilaya ya Singida wanategemea mafanikio makubwa kama walivyotegemea.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili (kushoto) akizungumza wakati wazira ya Mkuu wa Mkoa huo kujionea hali inavyoendelea kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoani hapo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo ameeleza kwamba changamoto ya kuishiwa chaji imejitokeza kwa Makarani wa Wilaya hiyo kwenye vijiji ambavyo havijapata huduma ya umeme.
Hata hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa katika Power benk zilizokuja Wilaya hiyo ipewe kipaumbele kwa kuwa pamoja na changamoto ya umeme kwa ajili ya kuchaji lakini bado kuna umbali wa nyumba hadi nyumba.
Kizigo amewataka wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuhakikisha kuendelea kuwa na subira kwa kukuwa katika kipindi cha siku Tano zilizobaki watahakikisha kila mwananchi anafikiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa huo kujionea maendeleo ya zoezi la Sensa katika mkoa wa Singida.
Aidha Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo amekiri kupokea power benk hizo ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa Makarani waliyopangiwa Vijijini ambapo hakuna Umeme.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.