MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Singida kuwapangia wakuu wa idara kila mmoja kusimamia mradi mmoja inayotekelezwa hivi sasa na wawe wanatoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi kila siku ili iweze kukamilika haraka kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Ametoa agizo hilo jana (Mei 29, 2023) baada ya kutembelea na kukagua miradi 12 katika Halmashauri ya Wilaya Singida na kubaini miradi inayotekelezwa wameachiwa walimu, Wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji na kata kuisimamia pekee yao hali iliyosababisha baadhi kasi ya ujenzi kusuasua.
Serukamba ambaye aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Singida (RAS), Dkt. Fatma Mganga, alisema Serikali imeleta fedha nyingi kwenye Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hivyo isimamiwe kwa ukaribu viongozi na wananchi waendelee kuhamasishwa kujitolea nguvu kazi ili iweze kukamilika haraka kwa wakati kabla mwaka mpya wa fedha haujaanza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili, alisema katika ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Murya kikwazo ni Mwenyekiti wa kijiji ambaye anazuia nguvu kazi za wananchi na kumhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba atalishughulikia suala hilo na kasi ya ujenzi itaongezeka.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.