• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Serukamba amaliza mgogoro wa shamba Yulansoni uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi.

Posted on: January 23rd, 2023

Uongozi wa Kijiji cha Yulansoni katika Kata ya Kinyangiri Wilayani Mkalama Mkoani Singida wameagizwa kuwarejeshea  wakulima mashamba wanayogombania  kwa kuwa hawana vielelezo vya kutosha vinavyoonesha kuwa  waliwakodishia wananchi hao mashamba hayo kwa mikataba.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo baada ya kukutana na viongozi na wazee wa Kijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mkalama.

Amesema yupo mwananchi ambaye ni mjane anayelalamikia kuzuiliwa kutumia ardhi yake ambayo alifyeka wakati likiwa shamba pori toka mwaka 1988 lenye jumla ya ekari 65 ambapo viongozi wa kijiji hicho walidai kwamba walimkodishia kwa mkataba wa miaka nane (8) jambo ambalo RC Serukamba alitaka Ofisi ya Kijiji kuwasilisha muhutasari wa vikao  na mkataba wa makubaliano hayo.

Aidha, Kijiji kiliwasilisha bàadhi ya nyaraka ambazo baadhi zinaonesha maandishi ambayo yanamtaja mjane huyo badala ya mume wake ambaye ndio alikuwa mmiliki wa shamba hilo, ambapo  RC Serukamba alisoma nyaraka hizo na kuonekana ziliandikwa mwaka 2005 badala ya 1998 ambapo marehemu ndipo alipofyeka shamba hilo.

Hata hivyo upande wa mlalamikaji uliendelea kudai kwamba Kijiji hicho kinahitaji shamba hilo ambalo sio mali yake ili kulikodisha ambapo tayari walishachukua fedha ambapo wanatakiwa akimkabidhi shamba au kurudishiwa fedha zake.

Kwa upande wake OCD wa Mkalama alikiri kwamba walipata malalamiko ya mwananchi huyo dhidi ya Kijiji cha Yulansoni ambapo walibaini mwananchi huyo aliachiwa shamba hilo na marehemu mume wake ambaye naye alipata kwa kufyeka pori huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Mesos akieleza kwamba aliwakutanisha mdai na mdaiwa ambapo maelezo ya wote wawili yanabainisha kwamba mwananchi huyo anamiliki eneo hilo.

Kutokana na maelezo hayo RC Serukamba aliwataka viongozi hao kuliachia shamba hilo kwa mwananchi huyo aweze kuendeleza shughuli zake za kilimo na kama hawajaridhishwa na uamuzi huo waende Mahakamani.

Naye Miwani wa Kata ya Kinyangiri Emanuel Kabea alimuomba RC kutembelea eneo lingine ambalo na lenyewe lina migogoro na Kijiji ambapo mwananchi aliyefahamika kwa jina la Edward Mnoma alichukua shamba hilo lenye ukubwa wa ekeri Mia moja (100) ambalo lilikuwa ni eneo la hifadhi ya Msitu wa Kijiji na akaliuza ambapo kwa sasa limebaki ekari 30 tu.

Aidha Diwani huyo amemuomba RC kutembelea eneo hilo na kuona kama ekari hizo 30 zilizopo  zinaweza kubaki katika umiliki wa Kijiji hicho jambo ambalo RC Serukamba aliahidi kutembelea eneo hilo baada ya wiki ijayo kupita.

Wakimalizia mjadala huo viongozi hao wa kijiji walimueleza Mkuu wa Mkoa huyo kwamba watarejesha shamba hilo kwa mlalamikaji huku wakijipanga ili kwenda kutafuta haki yao Mahakamani.

Mjadala huo ni muendelezo wa zoezi la utatuzi wa kero za Wananchi zilizotokana na ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoa huo ambapo aliwasikiliza wananchi kwa kipindi cha Siku nne mfululizo.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.