• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERUKAMBA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WATENDAJI ILI KUKABILIANA NA UGONJWA WA MLIPUKO

Posted on: November 7th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewaagiza Viongozi na Watendaji Mkoani humo kuhakikisha kaya zote zinakuwa na vyoo bora na kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria dhidi ya kaya ambazo hazina vyoo ili kukabiliana na ugonjwa wa mlipuko wa kuharisha na kutapika.

Akizungumza leo tarehe (7 Novemba, 2023) kwenye kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Serukamba amesema maradhi hayo husababishwa na mazingira ya uchafu hivyo jamii inapaswa kuhakikisha mazingira yote yanayowazunguka yanakuwa safi kwa lengo la kudhibiti magonjwa ya mlipuko hasa Kipindupindu ili kisiwepo kabisa Mkoani Singida.

Aidha, Serukamba amewasisitiza Wakuu wa Wilaya wote Mkoani humo kuhakikisha maeneo yote ya kaya, taasisi za umma, mashirika ya dini, masoko, stendi za mabasi, mashuleni, kwenye nyumba za ibada na mikusanyiko rasmi na isio rasmi kuwa na vifaa vya kunawia mikono, maji safi na sabuni ili kujikinga na maradhi hayo.

Amewasisitiza Wakuu hao wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maeneo yote ya kupikia na kuuzia vyakula yanakaguliwa na wataalamu wa Afya ili kuwa safi muda wote. Aidha kila Halmashauri ifanye kikao cha kamati ya Afya ya Msingi pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Hata hivyo Serukamba, amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SUWASA), Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa Singida (RUWASA) pamoja na Mkurugenzi wa Bodi Bonde la Kati kuhakikisha wanachukuwa sampuli za maji na kutibu visima vifupi, virefu na kusambaza maji safi na salama kwa watumiaji maji hayo ili kujikinga na ugonjwa huo wa kuharisha na kutapika.

Katika hatua nyingine, amewahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha maeneo yote ya minada na masoko yanakuwa na vyoo bora ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa huo wa mlipuko wa kuharisha na kutapika hasa katika Mkoa wa Singida.

Akimalizia maagizo yake Mkuu wa Mkoa huyo amewaagiza Waganga Wakuu wa kila Halmashauri kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na magonjwa ya kuharisha na kutapika kwa kutumia mikusanyiko ya hadhara, radio zilizopo ndani ya Mkoa, kutumia magari ya matangazo sambamba na kuhakikisha wanaopata dalili za ugonjwa wanawahi katika vituo vya huduma za Afya kwa ajili ya matibabu.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.