• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERUKAMBA AWAKOSHA WAKULIMA WA ALIZETI SINGIDA

Posted on: September 27th, 2022

Jumla ya kilo Mia tano (500) za mbegu bora za alizeti  aina ya Certified 1 zenye thamani ya Tsh. Bilion 2.5 zimetengwa kwa ajili ya kugawiwa wakulima wa mkoa wa Singida  ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kupunguza uagizaji wa mafuta toka nje ya nchi.

Akihutubia wananchi na wakulima wa Wilaya ya Iramba leo tarehe 27.09.2022 katika viwanja vya Halmashauri ya wilaya Iramba Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba amesema  Mbegu hizo zenye ruzuku ya Serikali zitauzwa kwa bei ya Shilingi Elfu tano (5,000) kwa kilo moja badala ya Tsh. 8,000.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki Kongamano la uzinduzi wa msimu wa Kilimo 2022/2023 wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa mbalimbali.

Aidha amesema Serikali itatao ruzuku ya mbolea kwa wakulima wote watakaojiandikisha kwenye mfumo maalum wa kupata ruzuku ambapo mfuko wa kilo 50 wa UREA NPKs na DAP utauzwa kwa  Tsh. 70,000 badala ya Tsh. 124,734 wakati CAN itauzwa kwa Tsh. 60,000 badala ya 131,676 na SA Tsh. 50,000 badala ya 82852.

Aidha Serukamba amesema kwamba katika bajeti ya mwaka 2022/23 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu katika miradi ya umwagiliaji Wilaya ya Iramba katika bonde la wembere linalounganisha Wilaya ya Ikungi na Iramba na Wilaya ya Mkalama ambapo kutakuwa na ujenzi wa skimu ya umwagiliaji na bwawa katika kata ya Msingi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiendesha Trekta ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa kongamano la uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 katika uwanja wa ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba

Hata hivyo RC Serukamba amesema kwamba njia pekee ya kuondoa umaskini, kuondoa uhaba wa mafuta ya kula na kuongeza usalama wa chakula nchini ni kukuza kilimo kwa kuiongeza eneo la uzalishaji wa kilimo cha umwagiliaji ambapo kutasaidia kuongeza ajira na upatikanaji wa mali ghafi za viwandani.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya siku ya ufunguzi wa Kongamano la uzinduzi wa Msimu wa Kilimo 2022/2023.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda amesema lengo la kongamano hilo ni kuonesha wakulima njia ya kutatatua changamoto walizokumbana nazo msimu uliopita kwa kuwa wana jukumu la kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti na Pamba na kuwaondolea wananchi umaskini.

Amesema wamewaalika Makampuni 16 ya uzalishaji na usambazaji pembejeo za kilimo wauzaji na wakopeshaji wa matrekta pamoja na mabenki mbalimbali ili waweze kutoa muongozo wa upatikanaji wa pembejeo na mikopo kwa wakulima wa Iramba.

Naye Afisa kilimo na ufugaji wa Wilaya ya Iramba Marietha Kasongo amebainisha kwamba Wilaya imelenga kulima hekta 127,594 za mazao ya chakula na hekta 134,176.4 za mazao ya biashara.

Aidha Kasongo ameeleza kwamba Wilaya ya Iramba inakabiliwa na changamoto za uzalishaji mdogo wa mazao kunakosababishwa na upatikanaji hafifu wa mbegu bora za mazao, matumizi hafifu ya zana za kilimo na uwepo wa visumbufu vya mazao.

Changamoto nyingine ni wakulima kutozingatia matumizi ya kanuni bora za kilimo upungufu wa wataalamu, miuondombinu mibovu ya umwagiliaji na mabadiliko ya tabia ya nchi alisistiza Marietha Kasongo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.