Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri pamoja na Takukuru wametakiwa kushirikiana ili kuondoa aina zote za rushwa ikiwemo rushwa ya ngono katika upatikanaji wa ajira mkoani Singida.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati akihutubia Wafanyakazi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei mosi) iliyofanyika katika uwanja wa Liti mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akihutubia Wafanyakazi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei mosi) iliyofanyika katika uwanja wa Liti mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa alibainisha hayo wakati akijibu risala ya chama cha Wafanyakazi mkoani hapo ambapo walibainisha uwepo wa rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi katika zoezi la upatikanaji wa ajira.
RC Mahenge alisistiza kwamba katika kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi mkoani hapo watumishi wanapaswa kuachana na mambo ya rushwa. "Takukuru nawaagiza mshirikiane na Waajiri pamoja na vyama vya wafanyakazi mkoani hapa ili kuondoa aina zote za rushwa ambazo zinaonekana pamoja na zile zilizosomwa katika risala na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoani hapa" alisema RC Mahenge.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa huo Dorothy Mwaluko aliwataka Wafanyakazi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuweza kuwatumikia Wananchi kama inavyotakikana.
Amesema kudai mishahara na marupurupu kuendane na utekelezaji wa majukumu yaliyo bora ili kuleta usawa wa vyeo na mishahara kulingana na mishahara inayotolewa.
"Nimeona Watumishia wa Serikali Mkoani hapa mkicheza kwaito na mkienda kwa Stepu kwa kupokezana bila kukosea ikionesha umahiri mlionao Katika mchezo huo, niwaombe Stepu hizo zitumike Katika kuwahudumia Wananchi katika ofisi zenu. Alisema Dorothy Mwaluko katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza na Wafanyakazi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei mosi) iliyofanyika katika uwanja wa Liti mkoani Singida
Shamrashamra mbalimbali zikiendelea wakati wa Sherehe ya Mei mosi mkoani Singida
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.