• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Singida na Mkakati wa kuondoa uhaba wa mafuta ya kula

Posted on: October 19th, 2021

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Binilithi Mahenge ametembelea mashamba makubwa yanayoandaliwa kwa ajili ya Kilimo cha alizeti wilayani Ikungi na kuzindua Msimu wa Kilimo kwa mwaka 2022 kwa wakulima wa kata ya Issuna wilayani hapo.

Akiwa katika mashamba hayo wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa  cha  pamoja (block farming) katika eneo lenye ukubwa wa Ekari 4800.

Amesema mashamba hayo makubwa ni maalum kwa ajili ya kilimo cha alizeti chenye lengo la kusaidia kupunguza tatizo la mafuta ya kula hapa nchini.

Ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wakulima upatikanaji wa matrekta kwa gharama nafuu yatakayo wasaidi kusafisha mashamba hayo.

RC Mahenge amebainisha kwamba  Serikali tayari imeleta mbegu ya kutosheleza mahitaji ya wakulima waliojiandikisha kwa kilimo hicho ambapo zitagawiwa kwa wakulima hivi karibuni.

Aidha amesema Serikali ya Mkoa itakutana na Benki ya NMB kujadili namna ambayo wataweza kusaidia usafishaji na uendeshaji wa mashamba hayo ambayo tayari wakulima hao wamekwisha jiunga na ushirika.

Akizindua msimu wa kilimo amesema RC Mahenge amewataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka  na kuongeza uzalishaji wa alizeti itakayotosheleza kulisha viwanda vya ndani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Jerry Muro amemueleza mkuu wa Mkoa kwamba  shamba hilo lina ukibwa wa Ekari 4500 zilizogawanywa Katika vipande  vya Ekari 100.

DC Jerry ametoa wito wa wawekezaji kuwekeza katika ujenzi wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia wakati wakulima wakisubiria soko na taratibu nyinginezo.

Aidha DC huyo amewataka vijana na akina mama kutumia fursa hiyo kushiriki katika kilimo, kuwekeza katika maduka ya pembejeo na pasitokee mtu kuzurula kwa kuwa utajiri umesogezwa mikononi mwao.

Hata hivyo Halmashauri ya Ikungi imedhamiria kuwasaidia wakulima hao wa alizeti katika mashamba makubwa kuwaunganisha na wenye zana za kilimo kwa ajili ya kusafisha maeneo hayo kwa gharama nafuu.

Katika hatua nyinge Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge walitembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Mang'onyi iliyopo Kijiji cha Mwalu Kata ya Mang'onyi ili kusikiliza changamoto zinazowakabili wakulima wa skimu hiyo.

Skimu ya Mang'onyi inahudumia vijiji vitatu vya Tupendane, Mwau na Mang'onyi yenyewe ambapo ina ukibwa wa hekta 450 lakini zinazotumika ni hekta 50 ambazo ndio zeye miundombinu ya umwagiliaji.

Akiongea na wanakijiji wa maeneo hayo Dkt.Mahenge ameagiza mashamba pori yote katika eneo la skimu hiyo yasafishwe na kufanyiwa kazi zilizokusudiwa.

RC. Mahenge amesema kila mmiliki wa shamba katika skimu hiyo ahakikishe analiendeleza, vinginevyo yatagawiwa kwa wakulima wengine wenye uhitaji.

Hata hivyo ameagiza wakulima wote wanaofaidika na Skimu hiyo kuchangia mfuko wa Umwagiliaji ambao umekuwa ukitumika katika kukarabati miundombinu ya Skimu inapoharibika

Amesema Skimu hiyo ikitumika kwa ufanisi ina uwezo wa kulisha Mkoa mzima wa Singida na mikoa ya jirani.

Akimalizia hotuba yake Mkuu wa mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi kutafuta fedha na kukarabati barabara inayoingia katika Skimu hiyo ili yawasaidie wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Wakiendelea na ziara  katika Skimu hiyo DC. Jerry Muro akawataka wanufaika kuhakikisaha wachague viongozi   ambao watasimamia na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji  kijijini hapo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.