• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SINGIDA YAADHIMISHA SHEREHE ZA UHURU KWA KUPANDA MITI ZAIDI YA 300

Posted on: December 9th, 2019

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Singida katika zoezi la kupanda miche mbalimbali ya miti zaidi ya 300 ikiwemo ya matunda, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya maadhimisho ya siku ya uhuru kitaifa mkoani Singida, kwa mwaka huu.

Shughuli hiyo ilianza mnamo majira ya saa 2 asubuhi kwa wananchi na viongozi wa Dini, vyama vya Siasa na Serikali kukusanyika katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ‘Mandewa’  kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la upandaji miti lililodumu kwa takribani masaa 3.

Akizungumza kwenye eneo hilo, Dkt. Nchimbi alisema taifa lolote la watu wabunifu, wazalendo na wawajibikaji ni lazima kwanza kuzingatia uwepo wa mazingira safi na salama yanayozunguka pande zote.

Alisema haikubaliki hata kidogo kwa baadhi ya watanzania kuendelea kukata miti kwa kisingizio cha kutafuta fedha au kujiajiri, huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kukosa uzalendo.

“Kwa maadhimisho haya sote tukubaliane kuanzia sasa kukata miti iwe basi…kiasi cha mkaa kinachokatwa Singida ni kikubwa, inasikitisha sana kuendelea kuona uharibifu huu mkubwa wa mazingira ukiendelea kufanywa ndani ya mkoa wetu,” alisema Nchimbi

Aliwataka wanasingida kuendelea kushikilia kauli mbiu iliyozoeleka ya mkoa huo ya ‘Achia Shoka kamata Mzinga’ kama sehemu ya kutunza misitu kwa ustawi wa afya ya mazingira na kiini cha ufugaji na uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa maendeleo ya uchumi wa kaya na taifa.

Akizungumzia kuhusu zao la korosho, Dkt. Nchimbi alisema zao hilo ni fursa ya kipekee ndani ya mkoa wa Singida kwa sasa, kwani ndani ya mda mfupi ujao linakwenda kubadilisha kabisa uchumi wa mkoa huo kutokana na wataalamu kuthibitisha kuwa zao hilo lenye thamani kubwa kuwa ni rafiki kwa ardhi ya mkoa huo.

“Tusichelewe kuifikia fursa hii itakayotusaidia kuimarisha uchumi wetu, hivyo naagiza kuanzia sasa kila mtendaji afanye sensa ya vijana waliopo kwenye maeneo yao, na hatimaye nataka kila kijana awe na walau nusu heka ya shamba la mkorosho,” alisema Nchimbi

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Dkt. Deogratias Banuba, alisema idadi ya miti hususani ya matunda iliyopandwa kupitia maadhimisho hayo italeta manufaa makubwa kwa ulaji na ustawi wa afya ya wagonjwa watakaoendelea kuletwa kwa matibabu hospitalini hapo.

Dk. Banuba ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji, akizungumzia kuhusu miaka minne ya uongozi wa Rais Magufuli ndani ya sekta ya afya, alisema kwa sasa huduma zimeboreshwa sana ikilinganishwa na hapo awali.

Alisema kwa upande wa huduma za upasuaji hasa kwenye eneo lake la mifupa huduma zote tena kwa kiwango cha juu kwa sasa zinafanyika ndani ya mkoa huo, huduma zimeboreshwa, vifaa tiba vyote muhimu kwa ajili ya mifupa vinapatikana tena kwa wakati.

Banuba alisema zamani walikuwa wakilazimika kuwapa rufaa wagonjwa ya kwenda kutibiwa hospitali za Dodoma au Muhimbili, lakini tokea Mheshimiwa Rais Magufuli aliposhauri Hospitali zote za Rufaa za mikoa zihamie Wizara ya Afya hakika kumekuwa na mabadiliko makubwa sana, hasa eneo la kibingwa.

“Sasa tuna huduma za upasuaji upande wa akinamama na kila eneo, kiukweli Singida kwa sasa tupo vizuri kwenye upande wa  sekta ya afya, na bado tunaendelea kuimarika zaidi kwa utoaji wa huduma bora na za viwango vya juu,” alisema Dkt. Banuba

Awali Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida (DAS), Wilson Shimo, alisema ukiachilia mbali zoezi la upandaji miti lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, kupitia tukio la kumbukizi hilo la miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, na 57 ya Jamhuri ya Muungano aliwataka wakazi wa mkoa huo kuwa makini na kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua.

“Niwasihi wananchi wote mnaoishi mabondeni, maeneo ambayo ni nyevu, chepechepe wachukue tahadhari ya kuondoka kwenye maeneo hayo, sambamba na kuwa karibu na watoto wadogo kwa kuepuka kuwaachia kutembea kwenye maji yanayotiririka au mito inayotembea kwa kasi au mashimo yaliyochimbwa kwa kina kirefu, ambayo yanaweza kuleta athari ya watoto kutumbukia na kusababisha vifo” DAS alisema

Alisema kwa neema ya mvua zinazoendelea kunyesha, aliwasihi wakulima kuendelea kutumia mvua zilizopo kulima kilimo cha kitaalamu kwa kuzingatia tija.

Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za uhuru kwa mwaka 2019 mkoani Singida.

Askali wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida wakishiriki kwenye shughuli ya kupanda miti kama shughuli maalum ya sehemu ya kumbukizi ya maadhimisho ya sherehe za uhuru kwa mwaka 2019 mkoani hapa.

Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victorian Ludovick (kushoto) akipanda mti kama sehemu ya kumbukizi ya maadhimisho ya sherehe za uhuru kwa mwaka 2019 mkoani hapa.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victorian Ludovick pesa taslimu kiasi cha shilingi 180,000 kwa ajili ya kuwapatia watoto wote waliozaliwa kwenye kumbukumbu ya siku ya uhuru kwa mwaka huu ndani ya Manispaa ya Singida.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victorian Ludovick akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wazazi waliojifungua siku ya maadhimisho ya uhuru, jumla ya watoto 12 waliozaliwa siku hiyo ndani ya Manispaa ya Singida  walipatiwa zawadi mbalimbali.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kofia ya rangi za bendera ya taifa) akiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali sambamba na wananchi wa mkoa wa Singida wakiomba dua ya kuombea Amani kwa mkoa huo na taifa muda mfupi baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti kama ishara ya kumbukizi ya maadhimisho ya sherehe za uhuru kwa mwaka 2019 mkoani Singida.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.