• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Takwimu za wananchi wanaopata chanjo mkoani Singida zaongezeka kwa kasi

Posted on: October 6th, 2021

Takwimu za wananchi wanaopata chanjo ya Uviko19 mkoani Singida zimeendelea kuongezeka kwa kasi kufuatia jitihada za utolewaji wa elimu na ushawishi kwa jamii kwa njia ya  nyumba kwa nyumba.

Akiongea wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Afya ya msingi (PHC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, RC Dkt. Binilith Mahenge amesema wiki mbili kabla ya kuanzishwa Mpango Shirikishi na Harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo ya Uviko 19 idadi ya watu waliokuwa wakijitokeza kuchanja ilikuwa 5800 mpaka 6000 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida kabla ya tarehe 22 Septemba mwaka huu.

Dkt. Mahenge amesema Mpango Shirikishi na Harakishi ambao uelimishaji ulikuwa unafanywa nyumba kwa nyumba  ulianza tarehe 22 Septemba  2021 katika Halmashauri zote saba 7 za Mkoa wa Singida ambapo ulisaidia kuongezeka idadi ya watu wanochanja  mpaka kufukia 11,847 ilipofika tarehe 5.10.2021 kwa Mkoa mzima.

Aidha Huduma ya mkoba na kliniki tembezi zimesaidia kuwafikia wananchi wengi katika minada mbalimbali mashuleni na maeneo ambayo hayakuwa na vituo vya kutolea huduma ya chanjo. Alibainisha Dkt. Mahenge.

Hata hivyo Dkt. Mahenge ametumia Kikao hicho kuendelea kuwaomba wadau na taasisi mbalimbali kusaidia upatikanaji wa usafiri wa kuwafikisha watoa huduma ya chanjo vijijini ili kuendeleza kutoa Kinga ya ungonjwa huo.

Amewataka wahudumu wa Afya na watumishi mbalimbali wanaohamasisha jamii kuhusu kuchanja na kuendeleza kufanya hivyo Mara kwa Mara kwa kuwa wananchi  wanakawaida ya kusahau.

Pamoja na mambo mengine wadau walikuwepo katika mkutano huo wamemuomba RC kushirikiana na wadau mbalimbali na mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea  kusaidia mapambano dhidi ya Ugonjwa huu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick katika taarifa yake amesema  kikao kilichopita waliadhimia kuendelea kutoa elimu ya chanjo na namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Uviko 19.

Dkt. Ludovick amebainisha kwamba wataendelea kuwatumia viongozi wa dini na  wanasiasa katika kupambana na Ugonjwa wa Uviko 19 kwa kuwa imeonekana kukubalika zaidi katika jamii zinazowazunguka.

Aidha uuzaji holela wa barakoa umeendelea kufanyiwa kazi hasa katika maeneo ya karibu na hospitali ambapo wapo wanaojaribisha kwa kuvaa barakoa hizo  kabla ya kununua hivyo kuweza kusababisha maambukizi. Alisema Victorina Ludovick.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama  mkoani hapa Mhe. Sophia Mfaume Kizigo amewataka wataalamu hao wa Afya kuongeza jitihada katika kutoa elimu maeneo ya mijini kwakuwa idadi kubwa ya waliochanja ipo Vijijini na sio mjini.

Hata  hivyo DC huyo alitoa wito kwa kila mwananchi aliyepata chanjo kuwa balozi wa kusaidia uhamasishaji kwa wengine.

Mwisho.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.