• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

TEKNOLOJIA KUTUMIKA KUFUNDISHIA WANAFUNZI MKOANI SINGIDA

Posted on: January 9th, 2025

Mkoa wa Singida umeweka mkakati wa kutumia teknolojia ya kufundisha masoko ya sayansi na Hisabati kwa kuziunganisha shule zote kwenye mtandao wa kompyuta ili Waalimu wachache waliopo wa masomo hayo waweze kufundisha shule nyingi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe.Halima Dendego  leo  wakati akihojiwa na kujibu maswali ya wananchi katika kituo cha redio cha Standard Radio ya mjini Singida katika kipindi cha "ZINDUKA" kuhusu mambo mbalimbali yaliyoyofanywa na serikali kwa mwaka uliopita na mikakati iliyopo kwa mwaka huu.

Amesema mkakati huo wa kutumia teknolojia kufundisha kwa masomo ya Sayansi na Hisabati ifikapo Juni mwaka huu 2025 shule zote hususani za Sekondari zitakuwa zimeunganishwa kwenye mtandao wa Kompyuta  na kwamba wamekuja na teknolojia hiyo kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa walimu.

"Tumekuwa na  upungufu wa walimu katika mkoa wetu hususani wa masomo ya Sayansi lakini Serikali kupitia Vyuo vya Ualimu imeendelea  kuzalisha walimu na Singida tumekuwa tukipata mgao wa walimu na tutahakikisha hakuna mtoto anayekosa somo fulani sababu ya upungufu wa walimu,"alisema Mhe.Dendego

Hata hivyo,Mhe.Dendego amesema ataitisha kikao na Waalimu kuzungumza nao kwani pamoja na upungufu uliopo maeneo ya mijini kuna idadi kubwa ya Waalimu huku  vijijini wakiwa wachache jambo ambalo litakwenda kupatiwa ufumbuzi ili kuweka uwiano sawa wa Waalimu katika shule zote kuanzia katika ngazi ya Kata na Vijijini.

Akizungumzia Kuhusu ukusanyaji wa mapato,alisema Halmashauri zinajitahidi sana kukusanya mapato ambapo katika robo ya kwanza zimekusanya asilimia 52 ambayo ni zaidi ya malengo  ya kukusanya ya  asilimia 50 na kuziagiza Halmashauri kuendelea kuongeza nguvu katika ukusanyaji hususani Halmashauri za Wilaya ya Iramba,Mkalama na Manispaa ya Singida.

Aidha,Mkuu wa Mkoa amewataka Wafanyabiashara kutoa stakabadhi za malipo kwa wateja wanaponunua bidhaa katika maduka yao ili kushirikiana na serikali katika mnyororo wa kukusanya mapato.

"Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali kwenye Mkoa wa Singida na sisi kama watendaji tutaendelea kusimamia kuhakikisha fedha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa," alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi hicho,msikilizaji aliyejitambulisha kwa jina la Mashaka Paul ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kuandaa mazingira mazuri ya kuwafikia wananchi katika kusikiliza na kutatua kero zao na kuahidi kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Singida katika mapambano ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa faida ya mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.