• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

TEMESA waagizwa kujitangaza ili kuongeza wateja

Posted on: March 29th, 2023

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga ameiagiza Taasisi ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kujitangaza kwa kufanya kazi zenye ubora na kutafuta wateja wapya badala ya kutegemea Serikali na Taasisi zake.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 29.03.2023  wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa TEMESA kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo zilizopo Singida mjini ambapo amesema Serikali imetoa mashine na mitambo mbalimbali kwa taasisi hiyo  ambazo zinaweza kuwa sababu ya kimbilio kwa wateja wa nje endapo huduma itaboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Dkt. Mganga ameagiza taasisi hiyo kufanya utafiti na kubaini sababu zinazosababisha upatikanaji hafifu wa wateja huku akibainisha kwamba uboreshaji wa huduma kwa mteja utasaidia kwa kiasi kikubwa Taasisi hiyo kufanya kazi ki biashara.

"Kwa vifaa ambazo Serikali imevileta tunategemea TEMESA iwe kimbilio kwa watu wengi, tangazeni kazi zenu muongeze wateja wa nje ya Serikali na hakikisheni mnaboresha huduma kwa wateja wavutiwe" Dkt. Mganga

Aidha amewataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuondoa malalamiko ambayo yalikuwepo awali yaliyohusu upatikanaji wa vipuri, matengenezo kuchukua muda mrefu na gharama kubwa ya matengenezo ambapo amewataka kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo na kununua vitu kwa pamoja (balk procurement) ili kupunguza gharama kwa wateja.

"TEMESA imeanzishwa ili kutoa unafuu wa utenegenezaji wa magari na umeme pamoja na mitambo kwa bei nafuu kuliko wengine hivyo niwapongeze kama mmeanza hatua za mabadiliko"

Hata hivyo RAS ameishauri Taasisi hiyo kupitia kitengo chake cha usimikaji wa umeme kuandaa mkakati wa kupima umeme katika majengo ya Serikali na  Taasisi mbalimbali na kutoa ushauri kwa wamiliki ili kuondoa changamoto za ajali za moto ambazo mara nyingi zimekuwa zikielezwa  kuwa zinasababishwa na hitilafu za umeme.

Hata hivyo  Dkt. Mganga amesisitiza watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu katika kutunza na kutumia mali za Umma na kuwekeza katika matumizi ya TEHAMA katika uhifadhi na ugawaji wa vipuri ili kuepusha upotevu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Hassani Karonda amesema katika kuboresha huduma zao Serikali katika mwaka wa fedha kwa mwaka uliopita ilitoa milioni 700 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu lakini ambapo kwa mwaka wa fedha ujao wametenga Bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza uboreshaji huo.

Awali akitoa taarifa ya kikao kazi hicho  Erasto Cheza fundi mkuu wa Karakana Mkoa wa Singida amesema majukumu ya karakana yao ni kufanya matengenezo ya magari pikipiki na mitambo ya Serikali, utenegenezaji na usimikaji wa mifumo ya Umeme na viyoyozi na ameendelea kueleza kwamba wanatoa ushauri wa kitaalamu nyanja za Mhandisi wa ufundi na umeme.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.