Mkoa wa Singida unatarajia kuvuna jumla ya tani 1,166,464.7 za mazao mbalimbali ya chakula yanayotarajiwa kulimwa kwenye hekta 585,744.9 katika msimu wa kilimo wa 2021/22 ndani ya maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida.
Kauli hii imetolewa leo 16.05.2021 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge katika kikao kazi cha uzinduzi wa ugawaji wa mbegu kupitia mradi unaofadhiliwa na mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwenye Sekta ya Kilimo uliofanyika katika ukumbi wa Socia Holl uliopo mjini Singida, ambapo amebainisha kwamba wakulima wamejiandaa ipasavyo katika msimu huu wa kilimo.
Akiwa katika uzinduzi huo Dkt. Mahenge amebainisha kwamba Mkoa unatarajia kupanda zao la mahindi katika eneo lenye ukubwa wa hekta 269, 175.6 ambapo matarajio ni kuvuna tani 501,526.3 wakati mpunga ukilimwa katika eneo la hekta 23,584.4 na kuvunwa tani 70,187.
Aidha mazao mengine ni mtama uwele ulezi ngano mihogo viazi vitamu na viazi mviringo ambavyo kwa jumla ya mazao yote kutatumika eneo lenye ekari 585,744.9 ambalo liltatoa mavuno kiasi cha tani 1,166,464.7 alifafa nua RC Mahenge.
Dkt. Mahenge amefafanua kwamba katika msumu huu wa kilimoa mkoa unatarajia kulima mazao mbalimbali ya biashara yakiwemo pamba , korosho, vitunguu, alizeti, Karanga, Choroko na Dengu ambapo eneo litakalolimwa mazao haya ni hekta 352,510.7.
Hata hivyo RC Mahenge akaendelea kufafanua kwamba katika msimu huu wa kilimo ,kwa upande wa mazao ya biashara Mkoa unatarajia kutoa mavuno yapatayo tani 955,200.5 ambapo wakulima na wananchi wa Singida watapata faida na kuongeza vipato na kuboresha maisha yao.
Awali akitoa takwimu za chakula Mkuu wa Mkoa amesema kwamba msimu wa mwaka jana eneo la Kilimo lilikuwa hekta 525 za mazao ya chakula zilizozalisha tani 821,881.7 ambayo ni ongezeko lililotokana na kuongezeka kwa tija katika kilimo iliyosababishwa na wakulima kutumia kanuni bora za kilimo.
Matumizi ya pembejeo na kanuni bora za kilimo zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kusaidia kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi wa mkoa wa singida alimalizia Dkt. Binilith Mahenge
Kikao hicho kiliwahusisha wizara ya Kilimo,wakuu wa Wilaya zinazolima alizeti, Makatibu Tawala wa mikoa ya Dodoma Singida,simiyu na Manyara pamoja na shirika la kimataiffa la kilimo (IFAD)
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.