Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge leo amefunga Mafunzo wakufunzi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Social uliopo mjijini hapo wakijiusisha wataalamu mbalimbali wa upimaji wa ardhi na wachora ramani kutoka maeneo mbalimba hapa Nchini.
Mafunzo hayo yalidumu kwa muda wa Siku kumi (10) na yalilenga kuwafundisha wataalamu namna ya kubadilisha data ziwe kijiditali ambapo watawafundisha wengine katika mikoa mbalimbali.
Akiongea katika Mafunzo hayo RC Mahenge amewataka vijana hao kutumia vyema mafunzo waliyoyapata ili taarifa hizo ziweze kutumika kikamilifu katika uwekaji wa anwani za Makazi.
Amewataka wakufunzi hao kutumia muda uliobaki kufikia Siku ya sensa kwa kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kutoa Mafunzo kwa wengine ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Naye Kamishina Msaidizi wa Ardhi Shamimu Hoza amesema kundi hilo la vijana baada ya Mafunzo hayo litasambazwa katika mikoa Saba ili kutoa elimu na kuendeleza kazi ya ubadilishaji wa taarifa kwenda katika digitali.
Aidha kundi hilo lenye vijana wapatao 47 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani linategemewa kuchochea mabadiliko makubwa katika kuyafikia malengo iliojiwekea alifafanua Kamishna
Amesema taarifa hizo zitasaidia kubaini maeneo ya makazi hifadhi na maeneo yenye matumizi mengineyo hasa katika kipindi hiki cha kuweka Anwani za Makazi alifafanua Shamimu
Hata hivyo Shamimu alimalizia kwa kuziomba taasisi nyingine kutoa ushirikiano au msaada wowote utakapohitajika hasa katika matumizi ya Tehama au endapo vitendea kazi vitaleta usumbufu wa aina yeyote.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.