• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

VIONGOZI WA KAMATI YA DINI MBALIMBALI MKOA WA SINGIDA WATOA SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2019

Posted on: December 24th, 2018

Viongozi wa Kamati ya Dini mbalimbali mkoa wa Singida wamewatakia Heri na Baraka wananchi wote wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla katika kipindi hiki cha Krisimasi na kuelekea mwaka mpya 2019, na kuwataka wananchi kusherekea kwa amani na utulivu.

Salamu hizo zimetolewa leo na viongozi hao walipokutana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na wameahidi kuendeleza maombi kwa nguvu zote kwa ajili ya kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt. John Joseph Magufuli na Tanzania, ili iendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Makamo mwenyekiti Askofu Kaale akisoma taarifa “Mwanadamu anapoishi hapa duniani hawezi akapata amani kutokana na vitu alivyonavyo kwa wingi kama fedha, dhahabu, magari, nyumba, mashamba na viwanja. Kwa sababu hiyo amani ya Mungu hupatikana kwa Mungu peke yake”

“Tunawahamasisha Watanzania na Singida yetu kwamba kila mtu ampe nafasi Mungu wa kweli amtawale ili kusababisha Amani ya kweli katika nchi yetu ya Tanzania”

Imedaiwa kuwa, amani na utulivu iliyopo nchini Tanzania, imechangia kwa kiasi kikubwa kwa Mheshimiwa Rais wa awamu ya TANO, Dkt. John Magufuli kuishangaza dunia kwa juhudi zake za kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya miaka mitatu.

Katika kuijengea nguvu hoja yao hiyo, Askofu Kaale, alinukuu Maandiko Matakatifu kutoka katika Biblia kitabu cha Isaya 32:17 inayosema “Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa utulivu na matumaini daima”.

“Sisi Kamati ya Dini mbalimbali hapa Mkoa wa Singida, tunaziona na kuzipongeza jitihada za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Magufuli”

“Ipo miradi mingi iliyotekelezwa na Serikali ndani ya miaka mitatu ya Rais Magufuli. Amesimamia misingi ya Uchumi, pamoja na changamoto kadhaa zinazoikumba uchumi wa dunia na hata ukanda wa Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara”

“Katika mwaka 2017/2018 uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.1 na kuifanya kuwa ya kwanza kwa Afrika Mashariki, lakini katika takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni ya Tisa kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi” Askofu Kaale akisoma taarifa.

Aidha, Viongozi hao kutoka Madhehebu mbalimbali ya mkoa wa Singida wamesema kwa umoja wao, wanaiunga mkoa Serikali ya Awamu ya Tano na kuwaasa watanzania kuendeleza utamaduni wa kulipa kodi ili fedha hizo zitumike kukamilisha miradi ya maendeleo katika taifa letu la Tanzania.

Naye kiongozi wa dhehebu la Kiislamu mjini hapa, Mbiaji Hassan, ametumia fursa hiyo kuyaomba madhehebu mengine yasiwe kikwazo kwa sikukuu hii ya Krismasi na kuelekea mwaka mpya 2019 na ameyasihi kuhakikisha sikukuu hizi zinasherekewa kwa amani na utulivu.

Hafla hiyo imehudhuliwa na mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Sweetbert Njewike.

Kwaupande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP, Njwewike, amewatoa hofu waumini wa madhehebu ya dini ya Kikristo na mengine na kwamba wamejipanga vema kuhakikisha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya zinapita vizuri bila kikwazo au usumbufu wa aina yoyote mkoani Singida.

Naye, Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, amesema ni ukweli usiopingika kwamba bei ya amani ni ndogo mno, lakini ikitoweka gharama yake ya kuirejesha ni kubwa mno.

“Kutokana na ukweli huo, natarajia kila mkazi wa mkoa huu uliopo jirani na makao makuu ya nchi anashiriki kuitunza na kuilinda amani na utulivu kama ilivyo kwa utamaduni wa mkoa wa Singida. Krismasi haipo kwa ajili ya kumuudhi mtu, ipo kwa ajili ya sherehe zinazotawaliwa na amani”, amesema Dkt. Nchimbi.

Hata hivyo, ametoa wito kwa familia kutumia sikukuu hizi kwa kukaa na familia zao ili kusherekea kwa amani na umoja na amesisitiza kwa wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao.

“Kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka ndicho ambacho familia zinatakiwa zikae na kutafakari mwaka mzima yote ambayo yamefanyika na ambayo tumekutana nayo, wapi tumekwenda vizuri, wapi hatukufanikiwa sana. Familia zikae pamoja zitafakari kwa pamoja na katika umoja wetu ni lazima tutashinda”

“Na unapokuta viongozi wa dini mbalimbali wanakaa pamoja na wanakuwa na nia moja na wanawafikia wananchi wao ambao ni waamini wao kwa pamoja, kwa vyovyote mahali hapo Mungu yupo”, Dkt. Nchimbi akielezea zaidi.

“Singida yetu ni Singida ya umoja, ni Singida ya upendo, ni Singida ya mshikamano, ni Singida ya amani, ni Singida ya utulivu na ni Singida ya maendeleo”

“Wakati huu wa Sikukuu ya Noel na mwaka mpya 2019, nawatakia Watanzania wote moyo wa Upendo, Furaha, Ukarimu na Amani kwa kila mtu,

KARIBUNI SINGIDA”. Dkt. Rehema Nchimbi.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.