• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Wadau wa Maendeleo Kutia Nguvu Kwenye Uhamasishaji na Elimu ya Chanjo Mkoa Wa Singida

Posted on: September 27th, 2021

Serikali imewapongeza Wadau mbalimbali wa maendeleo waliojitokeza katika kikao kazi cha Sekta ya Afya Mkoani Singida na kujitolea viwezeshi mbalimbali vitakavyosaidia  kuendesha zoezi la  utoaji wa  hamasa, elimu na chanjo kwa jamii .

Baadhi ya wadau hao wameahidi kusaidia upatikanaji wa  magari ya matangazo, mafuta kwa ajili ya safari za vijijini  huku wengine wakiwa tayari kusaidia kupeleka elimu waliyoipata kuhamasisha jamii juu ya  zoezi la uchanjaji lengo likiwa ni kufanikisha kwa kiwango kikubwa.

Pongezi hizo zimetolewa leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mganga Mkuu wa Mkoa  Dkt. Victorina Ludovick wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  Hoteli ya KBH na kubainisha kwamba  jitihada zinazooneshwa na wadu hao zitasaidia katika kuwafikia watu wengi vijijini na kutoa elimu ya chanjo.

Mganga Mkuu wa Mkoa  Singida Dkt. Victorina Ludovick akieleza jambo wakati wa mkutano huo

Pamoja na hayo Mganga mkuu amesema kwamba Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbalia  itaendela kusambaza huduma ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 katika maeneo mbalimbali Mkoani Singida kama hatua muhimu ya kupambana  na kudhibiti  ugonjwa huo.

Amesema Chanjo zinaendelea kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma ambapo awali vilikuwa  vituo 21 vilivyoanishwa na  Serikali lakini kupitia Mkakati Shirikishi na Harakishi, Serikali  itawafikia wananchi kupitia vituo 219 vinavyotoa huduma za Chanjo.

“Chanjo tayari zipo katika vituo vya kutolea huduma, lakini tunayo changamoto kubwa ya kufikisha elimu na hamasa ili wananchi wakubali kuzitumia” Alikaririwa Mganga Mkuu

Aidha amebainisha kwamba  jamii imekuwa na mwitikio mdogo katika kupokea  chanjo sababu kubwa ikiwa ni hofu iliyojengeka licha ya jamii kushuhudia wananchi wengine wakiendelea kunufaika  bila kuwepo kwa madhara yoyote.

Kutokana na muingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Mkoa wa Singida, Mikoa mbalimbali na Nchi nyingine, ni muhimu kuchukua tahadhari za kutosha ili kuukabili ugonjwa, Alibainisha Dkt Ludovick.

Aidha Dkt Ludovick. amesisitiza kwamaba Chanjo zilizoruhusiwa kutumika hapa nchini ni salama hivyo kila mtanzania ana hiari ya kupata chanjo hiyo na kuwataka kutokuwa na hofu .

Aidha amewataka Wadau wote na viongozi wa Dini kusaidia jitihada za Serikali ili Chanjo ziweze kuwafikia wananchi wote wenye uhiari wa kupatiwa Chanjo ili  kuiweka jamii salama.

Alimalizia kwa kusema kwamba Jukumu la kinga dhidi ya ugonjwa huu ni la kila mtanzania  hivyo kutoa wito kwa jamii kuendelea kuzingatia afua za kinga.

Hivyo, Wizara ya Afya inawataka Viongozi wote wa Serikali, sekta binafsi, Viongozi wa Kijamii na madhehebu ya dini kuwajulisha wananchi wote kuchukua tahadhari zote muhimu, kuelimisha, na kutekeleza afua za kujikinga .

Awali mratibu wa Malaria mkoani Singida Dkt. Abdalla Balla alieleza lengo la mkutano huo kwamba ni kutoa taarifa kuhusu hali ya UVIKO-19 na udhibiti wake katika Mkoa wa huo na  kubadilishana uzoefu pamoja na  kuyatambua  maeneo  Serikali iliyofanya vizuri.

Dkt. Abdalla aliendelea kusema mkutano huo utasaidia kuongeza ufanisi na ubora unaohitajika katika utoaji wa huduma za afya kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Serikali na kuwepo kwa mfumo mmoja wa utoaji huduma unaoshirikisha wadau wote ( mfumo wa rufaa – “Vertical and Horizontal referrals”)

Mwenyekiti wa dini mbalimbali Mkoa wa Singida Shehe Hamisi Mohamedi Kisuke akizungumza wakati wa mkutano

Naye Mwenyekiti wa dini mbalimbali Mkoa wa Singida Shekhe Hamisi Mohamedi Kisuke ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya chanjo hasa kwa vijana kwa kuwa katika kipindi hiki wameonekana kutokujali ugonjwa huku wengi wao wakiwa hawajapata chanjo.

Ameihakikishia Serikali kwamba kwa upande wa dini wanazo simamia wanaunga mkono na watashiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu ya chanjo kwa jamii kwa kuwa vitabu vya mwenyezimungu vinataka jamii kujikinga na mambo yenye kuangamiza. Alifafanua Shekhe Hamisi

Naye Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Singida Kati Rev.Gasper Mdimi amesema wamejipanga kuhakikisha wanashirikiana na Serikali kutoa elimu na hamasa juu ya chanjo ili kuwaepusha  Watanzania juu ya  madhara makubwa yanayoweza  kutokana na ugonjwa wa KOVID 19.

Mratibu wa Malaria mkoa wa Singida Dkt. Abdalla Balla akieleza lengo la mkutano huo

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.