• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

Posted on: May 30th, 2025

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amewataka wahitimu katika vyuo mbalimbali nchini kuepuka na vitendo vya rushwa na ufisadi wanapoajiriwa kwenda kufanya kazi kwakuwa mambo hayo yanaleta madhara katika ufanisi wa utendaji kazi wa Serikali.

Alisema  hayo leo wakati akizungumza na wanafunzi, watumishi na wananchi katika sherehe za mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Singida ambapo jumla ya wanafunzi 1330 walihitimu na kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali.

“Sote tunaohitimu katika vyuo vyote nchini mnapofikilia kwenda kufanya kazi serikalini mhakikishe mnakuwa wasimamizi na watunzaji wa maadili lakini pia mhakikisha mnatunza siri za serikali na mtaepuka rushwa na ufisadi na mambo mengine ambayo yanaleta madhala katika ufanisi wa utendaji kazi wa serikali,” alisema.

Simbachawene amesema duniani kote pamoja na kuwepo kwa rasilimali nyingine  lakini raslimali muhimu ni watumishi wa umma ambao wanapaswa kupata mafunzo kabla na baada ya kuanza kazi ili kuwajengea uwezo wa  utendaji mzuri wa kazi.

“Wakati mwingine tunalaumiana juu ya uwezo mdogo wa kiongozi wa chini lakini kumbe hawajapata mafunzo jinsi ya kuwahudumia wananchi, niwakumbushe na niwasisitize kwamba watumishi wa umma mnalo jukumu kubwa katika mchango wa maendeleo ya nchi, muhimu hapa ni kuhakikisha mnatunza maadili ya kazi,” amesema.

Simbachawene amesema nchi yetu ni kubwa ina wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali lakini ipo migogoro mingi hasa ya ardhi, hivyo watumishi wa umma  hususani maafisa watendaji wa vijiji, kata na tarafa wakijengewa uwezo jinsi ya kutatua migogoro itapungua na wananchi wataendelea na shughuli nyingine za uzalishaji badala ya kupoteza muda mwingi kwenye migogoro.

Aliongeza kuwa Serikali inayo matarajio makubwa na Chuo cha Utumishi wa umma na wahitimu wake katika kuhakikisha wanajenga uwezo na umahiri  katika katika kutekeleza majukumu yao wanapokuwa kazini.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatuma Mganga akizungumza katika mahafali hayo,Amewahimiza Wahitimu kutobweteka badala yake wajiendeleze katika fani zingine zinatolewa VETA ili waweze Kujiajiri.

"Sio dhambi kwa mtu aliemaliza Chuo cha utumish kujifunza fani mbali mbali,VETA kuna juzi nyingi,tusiende kukunja mikono na kuilaumu Serikali,kila mmoja ajishughulishe.Anaetaka ujuzi wa ufundi nenda kajiunge na VETA upate ujuzi wako wakati unasubiri ajira"amesema Daktari Mganga.

Naye Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk. Ernest  Mabonesho, amesema katika mafunzo ya muda mrefu chuo kimedahili wanafunzi 10, 507 katika ngazi mbalimbali na katika mafunz ya muda mfupi kimeweza kuwajengea uwezo watumishi 11,122 mpaka sasa na wale waliopewa mafunzo ya awali.

Amesema katika mwaka huu wa fedha unaoisha chuo kimefanya tafiti sita ambazo zipo hatua ya mwisho kukamilisha ambazo zinaangalia changamoto za uongozi katika usimamizi na ufanisi wa taasisi za umma na ufanisi wa mafunzo kwa watumishi wa umma katika kuwezesha kutoa huduma.

Dk.Mabonesho amesema tafiti nyingine zinazofanyika ni kuangalia maeneo ya Teknolojia na mabadiliko ya stadi katika kada ya uhazini, matumizi ya TEHAMA katika usimamizi wa shughuli za kiofisi,matumizi ya mfumo wa manunuzi wa kielektroniki katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi na  ufanisi wa utoaji wa huduma kwa upande wa Serikali za mitaa.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • ANUANI ZA MAKAZI KUJA NA FURSA LUKUKI ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

    May 26, 2025
  • WANAFUNZI NI SALAMA CHINI YA MRADI WA SHULE BORA .

    May 26, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.