• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WALIMU MKOANI SINGIDA WAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI YA PILI KITAIFA KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA HUU 2019.

Posted on: September 15th, 2019

SERIKALI ya Mkoa wa Singida imewapongeza walimu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali zilizopo mkoani Singida kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019 hadi kupelekea kushika nafasi ya pili kitaifa kati ya shule 29 zilizopo Tanzania bara na Visiwani.

“HONGERA SANA KWA MAFANIKIO MAKUBWA HAYA AMBAYO MUNGU AMETUWEZESHA”. Dkt. Rehema Nchimbi

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema, uwalimu ni wito, ni lazima uwe na uhusihano wa moja kwa moja na Mungu, kazi ya ualimu ni kazi Takatifu na sio kila mtu anaweza kuwa mwalimu.

Amesema, Mwalimu lazima awe mwenye huruma, mwalimu wakati wote lazima awe mlinzi katika nafasi pana. Mwalimu ni kiunganishi, anaunganisha ubao na darasa, anaunganisha yaliyopo kichwani kwake na wanafunzi.

“Ualimu ni usuruhishi, mwalimu ni mpatanishi, ukimuona mtoto hajapatanishwa vizuri na mazingira yanayomzunguka ujue kuna changamoto ya uwalimu” Dkt. Nchimbi

Amesisitiza kuwa, Saikoloji inasema hakuna binadamu asiyefundishika, hivyo, kufeli kwa mwanafunzi ni kufeli kwa mwalimu, “Mwalimu hata siku moja hafurahishwi na matokeo mabaya ya mwanafunzi wake bali hufurahishwa na matokeo mazuri (chanya) ya mwanafunzi wake”.

Aidha, ametoa wito kwa Wakurugenzi na Maafisa Elimu wa ngazi mbalimbali mkoani Singida kuwa karibu na walimu kwa kutenga muda wa kuwasikiliza pindi wafikapo maofisini kwao.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi, amesema Walimu ndio wanaoweza kututengenezea Taifa au kutuharibia, kwa sababu ndiyo wanaoshiriki katika malezi ya mtoto katika nyakati zote za makuzi yake.


Aidha, Dkt Angelina Lutambi, ametoa wito kwa walimu kujitokeza kwa wingi katika kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaaluma pindi yanapoandaliwa ili kuongeza tija katika sekta ya elimu mkoani Singida na Taifa kwa ujumla.

Naye, Afisa Elimu wa Mkoa wa Singida Mwl. Nelasi Mulungu amesema, mikakati iliyotumika na kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kila mwaka ni kufanya vikao vya pamoja na wakuu wa shule ambapo kila mkuu wa shule hueleza na kuwasilisha mikakati waliyojipanga kwa kila shule ambayo inahakikisha kuwa ufaulu unakuwa ni daraja la kwanza na la pili.

Aidha, Kufanya Majaribio kwa kila wiki, na baadhi ya shule wana wastani wa shule ambapo asiyeufikia wastani huo hupewa adhabu zenye kuwasukuma kuhakikisha kuwa kila mmoja anafanya vizuri mfano, kupewa mazoezi ya kutosha ili kuwafanya muda mwingi wawe wanajisomea.

Akisisitiza zaidi amesema, Wamefanikiwa kudhibiti utoro kwa kuhakikisha kuwa wakati wote wanafunzi wapo shuleni na darasani wanajifunza. Kuhakikisha kila mwalimu anakamilisha mada zote kwa wakati.

"Mkakati mwingine ni Kudumisha nidhamu kwa walimu na wanafunzi ili ufundishaji na ujifunzaji uweze kwenda vizuri na kwa kujituma". Mwl. Mulungu

Imetolewa na;

Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

SINGIDA

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.