• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Wanafunzi 28,072 kwenda Kidato cha kwanza, ni baada ya madarasa kukamilika mkoani Singida

Posted on: January 3rd, 2022

Jumla ya wanafunzi 28,072 waliofaulu mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2021 mkoani Singida watapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 kutokana na uwepo wa vyumba vya madarasa  zaidi ya 330 vilivyojengwa kwa fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa katika Halmashauri mbalimbali  mkoani hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyumba 662 vya madarasa na mabweni mawili iliyofanyika kimkoa Disemba 31, 2021 katika shule ya Sekondari Isuna, wilayani Ikungi.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati akikabidhiwa vyumba vya madarasa katika mkutano uliofanyika Kata ya Isuna wilayani Ikungi Disemba 31, 2021.

Akiwa katika mkutano huo RC Mahenge akamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa jumla ya Sh.Bilioni  13.4 kwa ajili ya  ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani hapa.

Dkt. Mahenge amesema mkoa ulikuwa na uwezo wa kupeleka wanafunzi wa Sekondari 11,520  pekee kwa wakati mmoja lakini baada ya fedha hizo jumla ya madarasa 330 yamejengwa  na wanafunzi 16,500 wa Sekondari wataanza shule mapema January 2022.

Aidha RC Mahenge akabainisha kwamba  ujenzi wa vyumba vya madarasa uliofanyika katika wilaya zote mkoani hapo zimetoa fursa kwa vijana na wakina mama kupata ajira kwa kushiriki kazi mbalimbali pamoja na kufanya biashara ya chakula kwa ajili ya mafundi na vibarua mbalimbali.

Muonekano wa moja ya vyumba vya madarasa yaliyojengwa mkoani Singida kupitia fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Akimalizia hotuba  yake Mahenge amewataka Wakurugenzi kuanza maandalizi ya kuendelea na ujenzi wa vyumba mbalimbali kwa kutumia fedha za ndani badala ya kusubiri msaada kutoka ngazi za juu.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko akimkaribisha Mkuu wa Mkoa ameeleza kwamba fedha zilizopokelewa kwa upande wa elimu zilikusudiwa kujenga vyumba vya madarasa 662 na mambweni mawili (2) ili kuweza kupokea wanafunzi wote kwa wakati mmoja.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla hiyo.

RAS Mwaluko amesema ubunifu mkubwa umefanyika katika ujenzi wa madarasa hayo ambapo tayari jumla ya ofisi 63 za walimu nazo zimekamilika ujenzi ambao haukuwepo kwenye mahesabu ya awali.

Amesema miradi hiyo imetoa funzo kubwa kwa watendaji kwa kuwa wameweza kutumia njia mbalimbali za kufanya manunuzi ikiwemo manunuzi ya pamoja (balk procurement) pamoja na changamoto zake ambapo amewataka wasimamisizi  wa miradi mbalimbali kuchanganua changamoto zinazojitokeza ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa ununuzi wa vifaa wakati mwingine.

Awali akitoa taarifa ya vyumba vya madarasa DC wa Ikungi  Jerry Muro  amesema walipokea Sh. Bilioni 2.64 za Miradi ya Maendeleo na Ustawi wa Taifa lengo likiwa ni kujenga  vyumba vya madara 132 ambavyo vimetekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo.

Dc Jerry Muro amefafanua kwamba  katika fedha hizo jumla ya Sh. Bilioni 1.3 zilitumika kujenga vyumba  67 katika shule za Sekondari 28 na Sh.Bilioni 1.3 zilitumika kujenga madara 65 katika shule  za msingi 16 ambapo jumla ya vyumba 132 vimekabidhiwa.

Aidha Jerry amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa katika kufanikisha zoezi hilo kwa kujitolea nguvu kazi hasa kwa kuleta mchanga, maji na kusomba vifusi jambo ambalo lilisaidia kukamilisha jukumu hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sindida Mhandisi Paskas Muragili akiendelea kutoa shukrani kwa Serikali amebainisha kwamba jumla ya wanafunzi 3,976 wanatoka Manispaa ya Singida watafaidika na ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.

Hata hivyo Mhandisi Muragili akaongeza  kwamba wilaya nzima ya Singida ina jumla ya wanafunzi 9,737 watakao nufaika na ujenzi wa madarasa wakiwemo 5791 kutoka Halmashauri za Singida vijijini.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo wakati wa  hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo wakati wa  hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo wakati wa  hafla.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo wakati wa  hafla.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo wakati wa  hafla.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba kwenye hafla hiyo.

Hafla ikiendelea

Muonekano wa ndani ya darasa lililojengwa kwa fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo.

Picha ya pamoja na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo

Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Singida wakiwa ndani ya moja ya darasa wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari ambapo zimesaidia kupunguza kero waliyokuwa wanaipata wananchi kwa kutozwa michango mbalimbali kwa ajili ya kukamilisha maboma na utengenezaji wa madawati hasa kipindi hiki ambacho shule zinakaribia kufunguliwa.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.