• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WANANCHI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Posted on: October 18th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amefanya ziara katika Halmashauri za Wilaya ya Iramba na Mkalama kwa ajili ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dendego amekutana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri hizo wakiwemo Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, Wasimamizi wa Uchaguzi, pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya uchaguzi huo.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kuhakikisha kuwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yanakwenda vizuri na kwamba wananchi wote wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo la kikatiba kwa amani, utulivu na uwazi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Dendego alisema:“Tunataka kuona Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika katika hali ya amani na utulivu. Viongozi wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi, wote tushirikiane kuhakikisha Singida inakuwa mfano wa uadilifu na utulivu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.”

Ameongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Singida imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu katika wilaya zote, halmashauri zote na mpaka ngazi ya kata, huku akihimiza viongozi na watendaji kushirikiana kwa karibu na wananchi katika kutoa elimu ya uraia na umuhimu wa kushiriki uchaguzi kwa amani.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Singida kuendelea kudumisha mshikamano na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama wakati wa mchakato wa uchaguzi.

Kadhalika Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga alifanya ziara yenye lengo sawa na hilo katika Wilaya ya Manyoni ambapo pia aliambatana na Viongozi wa Idara mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika nchini mnamo Oktoba 29,2025 ambapo utahusisha uchaguzi katika ngazi ya Rais,Wabunge na Madiwani.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

    October 18, 2025
  • MABINGWA WA CECAFA WAKARIBISHWA NYUMBANI BAADA YA USHINDI MNONO

    October 05, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WAWASILI SINGIDA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

    October 06, 2025
  • HALI YA HEWA YA MKOA WA SINGIDA YATAKIWA KUTUMIWA KAMA FURSA NA SIO KIKWAZO

    September 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.