• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Watendaji wa Makiungu, Mungaa Watakiwa kufanya "Data Cleaning" Katika zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi.

Posted on: May 9th, 2022

Watendaji wa Kata na Vijiji wametakiwa kufanya uhakiki wa namba za nyumba walizoweka  (data cleaning)  pamoja na vibao elekezi katika maeneo yao ya kazi  kabla ya kukamilisha na kukabidhi zoezi hilo kwa viongozi husika ili kuondoa dosari zilizojitokeza katika baadhi ya Kata wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa huo Dorothy Mwaluko akifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa  anwani za Makazi katika Kata za Makiungu, Mungaa na Siuyu katika Wilaya hiyo na kubaani changamoto ndogo ndogo zikiwemo uwekaji wa namba usiokuwa na Mpango mzuri pamoja na usimikaji wa vibao elekezi vyenye mbawa moja badala ya mbili.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa ziara hiyo

Akitoa majumuisho katika ziara hiyo amesema Wilaya  imefikia  hatua nzuri pamoja na uwepo wa changamoto chache zilizojitokeza ambapo amewataka Watendaji kuzikagua namba hizo na  kuziwasilisha kwa viongozi wao haraka ili kutafutiwa ufumbuzi wa haraka alieleza Dorothy Mwaluko.

Hata hivyo Mwaluko amewataka wananchi na wenyeviti wa vitongoji kuendelea kushirikiana na   waratibu wa anwani za Makazi ili kumaliza zoezi hilo kwa wakati.

Aidha, RAS akimalizia ziara yake katika kata hizo akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia muda uliobaki kujiridhisha na maeneo yaliokwisha tolewa taarifa kwamba yamekamilika  ili kujiridhisha ukamilifu wake.

Dorothy akaendelea kuwakumbusha Wakurugenzi hao kuhakikisha kila Taasisi zikiwemo mashule Misikiti, Makanisa na ofisi za watendaji kwamba zinakuwa na vibao vya anwani za Makazi.

Ziara hiyo iliwahusisha viongozi kutoka Jeshi la Magereza ngazi ya Mkoa, Jeshi la Uhamiaji Mkoa na Maafisa mbalimbali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Zoezi hilo pia lilifanyika katika Wilaya ya Manyoni na Halmashauri ya Itigi ambapo kamati ya ufuatiliaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo iliongozwa na Mshauri wa Jeshi la Akiba, Mkuu wa Takukuru pamoja na Mratibu wa Anwani za Makazi Mkoa ambapo iliwasisitiza Watendaji kuongeza kasi ya utekelezaji ili kufikia lengo tarajiwa pamoja na kuboresha namba za anwani za makazi na usimikaji wa vibao elekezi kwa ubora unaotakiwa.

Zoezi la ukaguzi wa usimikaji wa vibao elekezi na anwani za makazi ukiendelea wilayani Manyoni

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.