• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Watoto 292,857 kupata chanjo ya polio Mkoani Singida.

Posted on: April 11th, 2022

Mkoa wa Singida umedhamiria kutoa chanjo ya polio kwa jumla ya watoto  292,857 wa kuanzia umri wa Miezi 0 Hadi 59 ili kuzuia mlipuko wa Ugonjwa huo na kuongeza Kinga jamii  kwa watoto wote wa chini ya miaka mitano.

Akitoa wasilisho lake katika Kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhusisha wajumbe mbalimbali kutoka Halmashauri Saba za Mkoa huo, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wadau mbalimbali Mratibu wa chanjo mkoani Singida Habibu Said Mwinory amesema chanjo hiyo itatolewa kuanzia tarehe 21- 24 Aprili  2022 katika maeneo yote ya mkoa huo ambapo Kampeni hiyo itakuwa ya nyumba kwa nyumba na mtoto kwa mtoto.

Aidha bwana Habibu amesema idadi hiyo ya watoto wanaotegemewa kupata chanjo watatoka Halmashauri Saba za mkoa huu zikuhusisha Wilaya za Mkalama, Iramba, Singida DC, Ikungi, Manyoni na Itigi ambapo jumla ya chanjo 336,800 zinategemewa kutumika katika maeneo hayo.

Hata hivyo Mratibu huyo  amebainisha lengo la programu hiyo ya  chanjo ni kuongeza uelewa wa kutosha kwa watoa huduma na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kupata chanjo  dhidi ya Ugonjwa wa polio.

Hata hivyo Mratibu Habibu aliongezea kwamba idadi ya timu za wachanjaji, watunza taarifa pamoja na wahamasishaji wamefikia idadi ya watu 647 katika Wilaya zote Saba huku idadi ya vibebea chanjo vinavyohitajika vikiwa 647 sawa na idadi ya wahusika.

Aidha chanjo hizo tayari zimekwisha sambazwa katika maeneo mbalimbali ya vituo vya Afya katika Halmashauri zote Saba huku mafunzo yanaendelea kutolewa kwa wachanjaji watunza takwimu na wahamasishaji. Aliendelea kufafanua Mwinory.

Awali akitoa maelezo juu ya Ugonjwa huo Habibu amesema polio inaenezwa kupitia njia ya haja kubwa  kwa mtu kula au kunywa  vitu ambavyo sio salama ambapo Ugonjwa huweza kumpata mtu yeyote kàtika umri wowote ila mtoto chini ya miaka mitano huathirika zaidi.

Naye Mkuu wa Wilaya Singida Mhandisi Pasksi Muragili ametoa wito kwa wananchi wote mkoani hapa kushiriki zoezi hilo la chanjo salama ya kuzuia Ugonjwa wa polio kwa watoto chini ya miaka mitano huku akiwataka wazazi wenye Tabia ya kuwaficha watoto kuacha Tabia hizo Mara moja.

Aidha ameitaka timu iliyoundwa kwa ajili ya uhamasishaji kutumia vyomba vya habari kama mkakati maalum wa kufikisha taarifa hizo kwa watu wengi na  kutumia taasisi za dini kufikisha ujumbe kwa waumini wao.

Hata hivyo Mhandisi Muragili akaelekeza kushirikishwa viongozi wa ngazi za vijiji na Kata kwa kuwa wao ndio waliopo karibu na watu.

Afisa Lishe Mkoa wa Singida Bi. Teda Sinde akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo akizungumza wakati wa kikao hicho.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.