• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"WATOTO WANAOPATA LISHE WANAFABYA VIZURI DARASANI" MWL. DULENGA

Posted on: February 12th, 2026

Wazazi na walimu wameaswa kudumisha ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha elimu bora inaendelea kutolewa shuleni na kuleta matokeo chanya kitaaluma. Rai hiyo imetolewa leo tarehe 12 Februari 2026 na Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Bw. Makwasa Dulenga, wakati akishiriki mahafali ya kidato cha sita yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Ndago mkoani Singida.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Makwasa amesema mafanikio ya kitaaluma shuleni yanategemea mshikamano wa wadau wote wa elimu, hususan wazazi na walimu wenyewe. Amefafanua kuwa ushirikiano huo hujidhihirisha kupitia hatua mbalimbali ikiwemo uhamasishaji wa utoaji wa chakula shuleni, ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi na michango ya hiari inayowawezesha walimu wanaojitolea kuendelea kutoa huduma bora ya ufundishaji.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata lishe bora wakiwa shuleni, kwa kuwahimiza kuchangia chakula shuleni akisisitiza kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya lishe bora na ufaulu mzuri darasani. Amesema mwanafunzi anayepata chakula chenye virutubisho muhimu shuleni huwa na uwezo mkubwa wa kuzingatia masomo na kufanya vizuri katika mitihani.

Vilevile, Afisa Elimu amewahimiza wanafunzi kuendelea kuthamini fursa ya elimu kwa kujituma zaidi katika masomo yao, akibainisha kuwa wazazi na walezi wao wanajitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanawapatia mahitaji muhimu ya shule ikiwemo sare na vifaa vya kujifunzia ili kuwajengea msingi bora wa maisha ya baadaye.

Awali akiwasilisha taarifa fupi ya shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndago, Bi. Prisca T. Msemo, amesema wanafunzi wa kidato cha sita wanaohitimu wameonyesha kiwango kizuri cha maandalizi kitaaluma kupitia mitihani mbalimbali ya majaribio waliyoifanya, ikiwemo mtihani wa utimilifu (Mock) wa Mkoa wa Singida. Ameeleza kuwa katika matokeo ya mtihani huo, shule ilishika nafasi ya tano kati ya shule 27 za mkoa, ambapo wanafunzi 54 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 13 daraja la pili na mwanafunzi mmoja daraja la tatu, matokeo ambayo yanaonesha juhudi za walimu na wanafunzi pamoja na mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji yaliyopo shuleni hapo.

Kwa upande wa baadhi ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo wameipongeza hotuba ya mgeni rasmi na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika malezi na elimu ya watoto wao. Wamesema wataendelea kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kusoma ili waweze kufikia ndoto zao za kuendelea na masomo ya ngazi za juu. "Mgeni rasmi umesema maneno mazuri sana, umewahusia vijana wetu na sisi wazazi umetuhusia, basi tutashirikiana na walimu wetu. Pia nawashukuru walimu kwa kuwalea watoto wetu na ninyi watoto wetu bado kuna hatua huko mbele hivyo jitahidini katika masomo yenu sisi tuko pamoja na walimu wenu." Amesema mmoja katika wazazi.

Nao wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule hiyo wamewashukuru walimu wao kwa malezi bora ya kitaaluma na kimaadili waliyoyapata katika kipindi chote cha masomo yao shuleni hapo. Wamesema juhudi, moyo wa kujitolea na ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa walimu wao umekuwa chachu ya maendeleo yao darasani na nje ya darasa. Aidha, wameahidi kuwa watajituma kwa bidii katika mitihani yao ya mwisho ili kufanya vizuri zaidi na kuendeleza rekodi ya ufaulu wa shule hiyo, huku wakisisitiza kuwa wataendelea kuitunza heshima ya shule yao kwa matokeo mazuri yatakayodhihirisha ubora wa elimu waliyoipata.




Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • "WATOTO WANAOPATA LISHE WANAFABYA VIZURI DARASANI" MWL. DULENGA

    February 12, 2026
  • DINI NI NYENZO YA MAADILI, UMOJA NA UTIIFU WA SHERIA – DKT. FATUMA MGANGA

    February 08, 2026
  • RC DENDEGO ASISITIZA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA WADAU WA KILIMO.

    February 06, 2026
  • MAAFISA UGANI WAASWA KUWA WATATUZI KERO ZA WAKULIMA SHAMBANI

    February 02, 2026
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.