• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Watoto wenye umri wa miaka chini ya 15 Ikungi wanavyoshiriki vitendo vya wizi

Posted on: January 19th, 2023

Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wilayani Ikungi Mkoani Singida vimeagizwa kufanya msako wa kina na kuwabaini watoto wenye umri wa miaka hadi kumi na tano wanaotajwa kushiriki vitendo vya wizi na ukabaji wakati wa usiku pamoja na wezi wengine na kuwafungulia mashtaka ili kuondoa vitendo hivyo ambavyo inasemekana vimekithiri katika eneo la Kijiji cha Puma Wilayani hapo.

Maelekezo hayo yametolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba wakati akisikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani hapo Mkutano ambao uliofanyika katika viwanja vya wazi katika Kijiji cha Puma.

Amesema vyombo vya Ulinzi na Usalama vishirikiane kupeleleza na kufanya msako mkali kuhakikisha watoto hao wanakamatwa na wanafunguliwa mashtaka ili kukomesha tabia hiyo huku akiwakumbusha wazazi kushirikiana na vyombo hivyo kuwapata.

Aidha, RC amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu wanaoshiriki kuiba miundombinu ya barabara na umeme ambayo imesemekana inatumika kutengenezea mikokoteni na majembe ya kukokotwa na wanyama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Samweli Mdimu ameelezea kero hiyo kwamba walifanya msako na kukamata baadhi ya watoto hao ambapo wazazi wao walikiri kwamba hawana pa kuwapeleka.

Samweli aliendelea kumueleza RC Serukamba kwamba walipowakamata na kuwafikisha Kituo cha Polisi Maafisa wa Polisi walishauri waachiwe kwa kuwa walikuwa na umri mdogo hivyo wazazi wao waelezwe ili wawaonye.

Aidha wananchi hao wameomba Polisi kuongeza ushirikiano na wananchi ikiwezekana  kushirikiana na Mgambo  wakati wa kufanya doria huku wakiomba Kituo chao cha Polisi kufanya kazi masaa 24 ili kiweze kuwasaidia nyakati zote.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.