• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WATUMISHI SINGIDA WATAKIWA KUTUMIA MFUMO WA NeST KWENYE MANUNUZI YA UMMA

Posted on: August 22nd, 2023

WATUMISHI wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa mkoani Singida wametakiwa kutumia mfumo mpya wa ununuzi wa umma ujulikanao NeST ulioanzisha na Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) ambapo mtumishi akifanya manunuzi bila kutumia mfumo huo atakuwa ametenda kosa la jinai.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, alisema hayo kwenye mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka halmashauri zote za mkoa huu kwa siku tano na kuwaeleza kuwa kutumia mfumo huo ni jambo la lazima kwani ni maelekezo mahsusi ya Serikali.

Ludovick alisema mfumo huu mpya wa manunuzi ni dhahili utaleta uwazi zaidi katika taratibu za manunuzi na utaongeza tija kwenye shughuli za Serikali hasa kwenye fedha ambako sehemu kubwa ipo kwenye manunuzi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi Sekretarieti ya Mkoa wa Singida, Nkuli Nketo alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watumishi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ili waweze kutumia mfumo huo mpya kuanzia Oktoba Mosi 2023 kwa lengo la kuepuka kufanya manunuzi ya aina yeyote nje ya mfumo wa NeST ambapo mfumo ulivyojengwa utawawezesha watumishi kufanya manunuzi ya aina yeyote ndani ya mfumo.

MATUKIO KATIKA PICHA

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA mkoa wa Singida, Baraka Mhembano akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka halmashauri zote za mkoa huo.

Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi Sekretarieti ya Mkoa wa Singida, Nkuli Nketo, akitoa elimu ya matumizi ya mfumo mpya wa manunuzi (NeST) wakati wa mafunzo hayo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka halmashauri zote za mkoa huo.

Baadhi ya watumishi kutoka Mamlaka ya Serikali za mitaa wakiwa katika majaribio ya matumizi ya mfumo wakati wa mafunzo hayo. Kusho ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA mkoa wa Singida, Baraka Mhembano akifuatilia mafunzo hayo. 

  

Mafunzo yakiendelea.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.