WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa Kassim amesemakuna haja ya kuangalia upya mfumo wa elimu ya juu nchini ili kuuboresha uwezekusaidia kutayarisha haraka rasilimali watu walioelimika zaidi,watakaoliwezesha taifa kuwa na maendeleo na kufikia uchumi wa kati ifikapomwaka 2025.
Waziri MkuuMajaliwa ameyasema huyo jana wakati akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya33 ya Chuo Kikuu huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya KanisaKatoliki mjini Singida.
“Kwakuzingatia malengo ya dira ya taifa ya maendeleo na mwelekeo wa serikali ya awamuya tano, napenda nisisitize kuwa dira ya utendaji wenu ijikite katika maeneoyaliyoainishwa chini ya mwamvuli wa kauli mbiu ya chuo-elimu bora na nafuu kwawote”, amesema.
Amesisitizakwa kusema kwa uchumi wa kati na wa viwanda, hauwezi kufikiwa au kuwa endelevupasipo kuwa na kiwango cha udahili katika elimu ya juu cha angalau asilimia 23.
“Hivi sasakiwango cha Tanzania cha udahili katika elimu ya juu ni aslimia nne (4). Kiwangohiki ni kidogo hata kuliko nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaolicha ya hali ya vita nchini mwao kwa muda mrefu,wamefikia asilimia saba (7)”,amefafanua.
WaziriMkuu Majaliwa amefafanua zaidi kwa kusema kuwa takwimu zinaonyesha kwambakaribu nchi zote washiriki katika jumuiya ya Afrika mashariki, ukiacha Burundi,zina viwango vya juu zaidi vya udahili katika elimu ya juu ikilinganishwa nakiwango cha Tanzania.
Amesema kwa mujibuwa sera ya elimu ya mwaka 2014 mfumo wa elimu na mafunzo umetawaliwa na muundowa kitaaluma wenye dhana ya kuchuja wahitimu kwa kila ngazi ili kupata wachachewenye uwezo mkubwa katika taaluma.
“Hali hiiinatokana na nafasi za elimu na mafunzo ngazi za juu kuwa chache kadriwanafunzi wanavyohitimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na kuendelea. Kwauhaba wa nafasi za elimu ya juu na ufinyu wa bajeti ndio unaosababisha kutumiamuundo wa kuchuja badala ule wa kutoa fursa kulingana na uwezo, vipaji navipawa”, amesema na kuongeza;
“Huundio mfumo ambao unahitaji kuhuishwa na mfumo wa elimu huria na masafa kamaalivyoeleza Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia Profesa Joyce Ndalichako kwambamazingira, vigezo na masharti ya mchakato huu vimeainishwa katika sera ya elimuna mafunzo 2014’.
Wakatihuo huo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaunga mkono azma ya Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia ya kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuimarishamfumo wa elimu huria na masafa.
“Kupitia haflahii, ninaagiza dawati kama hili lianzishwe pia katika Tume ya vyuo vikuu (TCU)na Baraza la elimu ya ufundi (NACTE), kwa lengo la kuhakikisha kuwa taratibuzao za ithibati zinazingatia na kukidhi matakwa ya viwango vya mfumo wa elimuhuria na masafa”, amesema.
KatikaMahafali hayo Mkuu wa Chuo Kikuu Huria na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo PeterPinda amemtunuku shahada ya heshima ya uzamivu Balozi Nicolous Kuhanga ambayemchango wake umetajwa kuwa mkubwa hasa wakati wa kuanzishwa kwa chuo hicho.
Zaidiya wahitimu 2200 wamehitimu katika Chuo Kikuu hicho na kutunikiwa shahadambalimbali ambapo mke wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mama Mary Majaliwa, amekuwa miongoni mwawahitimu akitunukiwa shahada ya uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.