Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Singida Vijijini lililopo Kata ya Ilongero ambako limegharimu kiasi cha fedha Tsh. Bilioni 2.7 ambapo ameagiza jengo hilo kukamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma inayostahili.
Waziri Mkuu ameyasema hayo hivi karibuni baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo hilo na kufafanua kwamba Ujenzi huo unalingana na kiasi cha fedha kilichotumika ambapo aliwapongeza viongozi walioweza kulisimamia.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiweka jiwe la msingi Mradi wa Ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Singida Vijijini
Amesema jengo hilo ni miongoni mwa majengo ambayo yamekuwa yakitolewa fedha nyingi na Serikali ili kuwasaidia wananchi kupata huduma.
Katika Ujenzi huo kiasi cha fedha Tsh.700 zilizobaki Waziri Mkuu ameahidi kwamba zitakuja ili zitumike katika umaliziaji na Ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa Ofisi hiyo.
Hata hivyo Waziri Mkuu amempongeza Mkurugenzi wa Singida DC Ester Chaula kwa usimamizi wake katika kazi za Serikali huku akimtaka kuendelea kuwasimamia wagavi katika kununua vifa vya ujenzi kama alivyofanya awali.
Hata hivyo amewataka Watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii na kuwafuata wananchi vijijini ili kuwapa huduma na kuwaeleza fursa ambazo Serikali imekuwa ikizitoa.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa Singida Vijijini mara baada ya uwekaji jiwe la msingi Mradi wa Ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Singida Vijijini
Amesisitiza nidhamu katika kazi kwa Watumishi na viongozi wao kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa ni chanzo cha mafanikio.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema Serikali imeleta miradi mingi Mkoani hapo ambayo inatumia kiasi kikubwa cha fedha hivyo ameahidi kuzisimamia na kuhakikisha thamani yake ina onekana.
Aidha amewataka wananchi wa Singida kuitunza miradi hiyo ikiwemo miradi ya maji elimu na Barabara ambazo fedha nyingi zimetolewa na Serikali na kwa kufanya hivyo utaweza kuwasaidia watu wengi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) akizungumza na wananchi wa Singida vijijini wakati wa ziara ya uwekaji jiwe la msingi jengo la ofisi ya Halmashauri
Serukamba ameendelea kuwaeleza wananchi wa Ilongero dhamira yake ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima ya Afya ambayo itarahisisha kupata huduma za Afya kwa kila mwananchi.
Ziara ya Waziri Mkuu ililenga kukagua miradi mbalimbali ikiwemo jengo la ofisi ya Halmashauri ya Ilongero na upanuzi wa Hospitali ya rufaa ya Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto.) akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serikamba mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la halmashauri ya Singida Dc
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.