• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Waziri Ummy awataka Madiwani nchini kuacha mivutano isiyo na tija katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

Posted on: December 22nd, 2021

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, ameyataka mabaraza ya Madiwani nchini, kupitia vikao vyake kuhakikisha yanafanya maamuzi sahihi yenye tija kwa jamii, badala ya maslahi binafsi yanayosababisha mivutano isiyo na tija.

Mheshimiwa Ummy amesema hayo leo Disemba 22, 2021 wakati akikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Kata ya Ilunda, wilaya ya Mkalama mkoani Singida, ambacho Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wanapinga ujenzi wake wakitaka kijengwe Kata ya Gumanga huku maagizo ya Serikali yakiwa kijengwe Kata ya Ilunda.

Waziri Ummy, amesema kituo hicho ni muhimu kwa Kata ya Ilunda kutokana na eneo hilo kukosa huduma sahihi za afya kwa muda mrefu na kitahudumia Kata Nne zilizopo wilayani humo.

“Niwaombe waheshimiwa Madiwani tuache mivutano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo sisi tulichagua kituo cha afya kijengwe katika Kata ya Ilunda kwasababu kitahudumia Kata Nne. Tunaangalia kipi kitaleta tija ya haraka. Tunajua maamuzi yanafanywa na mabaraza ya madiwani lakini tufanye maamuzi yenye tija.” Amesema Mhe. Ummy Mwalimu

Aidha kutokana na mvutano huo uliokuwa ukichelewesha ukamilishwaji wa kituo pamoja na uidhinishaji wa fedha za ujenzi huo kutoka benki, Waziri Ummy akamwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko, kuhakikisha anachukua jukumu hilo, ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.

“Nafahamu mpaka leo (22/12/2021) Mwenyekiti amekataa kusaini mikataba ya ujenzi, Mimi nampa mamlaka Katibu Tawala wa Mkoa ya kusaini. Hatuwezi kuchelewesha ujenzi wa kituo hiki wakati fedha imekuja tangu mwezi wa Nane”. Alisisitiza Mhe. Ummy Mwalimu

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, amemhakikishia Waziri kuwa Ujenzi wa kituo hicho utakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na miradi mingine ya maendeleo inayoendelea kujengwa nkoani humo.

Hata hivyo amemshukuru na kumpongeza Waziri wa TAMISEMI kwa kuhitimisha ziara yake ya siku TATU ya kukagua Miradi ya maendeleo, Elimu, Afya na Miundombinu sambamba na kikao na Sekretarieti ya Mkoa pamoja na vikao na mabaraza ya Madiwani katika halmashauri za Mkoa.

Nao wananchi wa Kata hiyo akiwemo Hawa Gyimbi, Oscar Daudi na Josephine Maige, wamefurahishwa na uamuzi huo unaoenda kumaliza tatizo la kufuata huduma za afya umbali mrefu jambo ambalo lilikuwa likiwatesa kwa miaka mingi.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy, amewapongeza Watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkoa kwa jitihada walizozifanya kuhakikisha ujenzi huo unaendelea kwa kasi na kuwataka ukamilishwaji kwa wakati ili huduma za afya zianze kutolewa kwa wananchi hao.

Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama yenye jumla ya zahanati 34, vituo vya afya vinne na hospitali mbili, ilianzishwa mwaka 2013, baada ya kugawanya kutoka wilaya ya Iramba.

MWISHO.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.