• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NA WAVUVI SINGIDA ZAANZA KUPATIWA UFUMBUZI

Posted on: January 10th, 2026

Wananchi wa Wilaya za Iramba na Mkalama mkoani Singida wameeleza matumaini mapya baada ya ziara ya kikazi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Bashiru Kakurwa (Mb), iliyofanyika leo tarehe 10 Januari 2025, wakisema imefungua fursa ya kusikilizwa na kushughulikiwa changamoto zinazowakabili katika sekta ya mifugo na uvuvi.

Katika Wilaya ya Iramba, wananchi na viongozi wa wilaya walieleza kuwa uchumi wa eneo hilo unategemea kwa kiasi kikubwa ufugaji na uvuvi katika Ziwa Kitangiri. Mkuu wa Wilaya alibainisha kuwa wilaya ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado inakabiliwa na upungufu wa miundombinu ya kisasa kama machinjio, minada na majosho, pamoja na uhaba wa watumishi wa mifugo na uvuvi. Alisema hali hiyo imekuwa ikiwalazimu wananchi kutumia gharama kubwa kupata huduma na wakati mwingine kushindwa kufikia masoko yenye tija.

Afisa Uvuvi wa wilaya alieleza kuwa shughuli za uvuvi zinaendelea kufanyika licha ya changamoto za vifaa na rasilimali, akibainisha kuwa wilaya ina wavuvi hai 204, mitumbwi 34 iliyosajiliwa na boti moja pekee. Alisema bado kuna hitaji kubwa la kuimarisha usimamizi wa rasilimali za uvuvi, kutoa elimu ya uvuvi endelevu kwa wananchi na kuboresha miundombinu ya uvuvi ili kuongeza tija na kipato cha wavuvi.

Katika Wilaya ya Mkalama, Mkuu wa Wilaya alisema migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa changamoto ya muda mrefu, hasa katika maeneo ya mipakani, akisisitiza kuwa kuwekwa kwa mipaka rasmi kati ya Wilaya ya Mkalama na Meatu ni hatua muhimu ya kudhibiti migogoro hiyo. Aliongeza kuwa kuna haja ya kulifufua shamba la mifugo la Serikali lililotelekezwa na kuvamiwa, ili kulinda mali ya umma na kutoa mfano wa ufugaji wa kisasa kwa wananchi.

Wananchi wa Kijiji cha Nyahaa walieleza kero zao kuhusu uvamizi wa mifugo, wizi na migogoro iliyosababisha majeruhi na hasara za mali, wakisisitiza umuhimu wa Serikali kuchukua hatua za haraka kurejesha amani na kuimarisha ulinzi wa mifugo.

Kwa ujumla, wananchi walisema ziara hiyo imeongeza uwazi na matumaini mapya, huku viongozi wa wilaya na wataalamu wa sekta wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ili kuboresha huduma za mifugo na uvuvi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Singida.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MADIWANI WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI,MAPATO NA NIDHAMU KWA WATUMISHI

    January 15, 2026
  • CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NA WAVUVI SINGIDA ZAANZA KUPATIWA UFUMBUZI

    January 10, 2026
  • WANANCHI WAGUSWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA KISHERIA MKOANI SINGIDA

    January 09, 2026
  • MIFUMO YA KIDIGITALI KUWAFUNGULIA MILANGO WAJASIRIAMALI

    December 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.