Seksheni ya Afya na Ustawi wa Jamii
Seksheni hii inajumuisha na hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, lengo la seksheni hii ni kusaidia au kuwezesha utoaji wa huduma bora za Afya za kinga, matibabu na maendeleo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii katika Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya seksheni/sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii:
TATHMINI YA HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA, USTAWI WA JAMII NA LISHE MKOA WA SINGIDA
Mkoa wa Singida una wilaya tano (5) ambazo ni: Ikungi, Iramba, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri saba (7) ambazo ni: Halmashauri za Wilaya Ikungi, Iramba, Itigi, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri ya Manispaa ya Singida. Aidha, Mkoa una jumla ya Tarafa 21, Kata 136, Vijiji 441, Mitaa 53 na Vitongoji 2,298. Kwa mujibu wa taarifa ya makadirio ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2021, inakadiriwa Mkoa wa Singida kuwa na idadi ya wakazi wapatao 1,754,370 wanaojumuisha Wanaume 868,646 na Wanawake 885,724.
Huduma za Afya zimeendelea kutolewa kwa kuzingatia Sera, Miongozo na kanuni mbalimbali za Afya katika afua zote za Tiba na Kinga. Mkoa una jumla ya vituo 256 vya kutolea huduma za Afya ikiwa ni Hospitali 11 Vituo vya Afya 20, Zahanati 221 na kliniki 4.
Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoa wa Singida
|
Serikali |
Mashirika |
FBO/NGO |
Binafsi |
Jumla |
Hospitali
|
5 |
0 |
6 |
0 |
11 |
Vituo vya Afya
|
18 |
0 |
1 |
1 |
20 |
Zahanati
|
189 |
0 |
25 |
7 |
221 |
Kliniki
|
0 |
0 |
1 |
3 |
4 |
Jumla
|
212 |
0 |
33 |
11 |
256 |
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.