• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

AGIZO LA MHE. RAIS LA KUWATAMBUA NA KUWAPATIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO LAANZA KUTEKELEZWA MKOANI SINGIDA

Posted on: December 17th, 2018

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. REHEMA NCHIMBI ametekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, la kutoa na kuwagawia vitambulisho vya kuwatambua wajasiriamali wadogo wenye mauzo ghafi yasiyofikia kiasi cha shilingi milioni 4 kwa mwaka.

Akikabidhi vitambulisho hivyo mkoani Singida, Dkt. Nchimbi amewataka wafanyabishara hao kutumia fursa hiyo vizuri kwa kufanya biashara kwa nidhamu na uadilifu mkubwa kama hatua ya kuboresha maisha yao pamoja na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.

“Mkivipata vitambulisho hivi, lazima kukivaa wakati wote katika shughuli zenu za kibiashara. Hazuiwi mjasiriamali eti kwasababu amepatia mkoani Singida basi abaki Singida, anauhuru na anahaki ya kwenda kufanya biashara mahali popote hapa nchini ilimradi popote atakapokuwapo avae kitambulisho hiki”. Amesisitia Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi alisisitiza, Mmachinga aliyepata kitambulisho afanye biashara yake kifua mbele bila kubughudhiwa na mamlaka yeyote.

“Ndugu zangu Wamachinga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli anawapenda sana wananchi wake na amesikia kilio chenu ambapo mlikuwa mkinyanyaswa na kubughudhiwa. Lakini kwa sasa mko huru ilimradi mna vitambulisho vyenu ambavyo mtakuwa mmevivaa shingoni hakuna mtu atakayewabughudhi”.

“Viambulisho hivi haviuzwi bali vinachangiwa kwa kila Mmachinga shilingi elfu ishirini na unaweza kuvitumia mahali popote nchini na vinatolewa na ofisi za wakuu wa Wilaya, hivyo natoa wito kwa Machinga wote katika Halmashauri za mkoa wangu wa Singida ili kuwaondolea bughudha zinazowakabili wanapokuwa wakiuza bidhaa zao Machinga hawa wasisumbuliwe wala kubughudhiwa”. Alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Nchimbi amewalipia vitambilisho hivyo baadhi ya Machinga wenye uhitaji maalum (walemavu) na viongozi wa dini mbalimbali za mkoani hapa ambao wamekidhi vigezo vinavyotakiwa na Serikali vya mtu kuwa Machinga. Pia aliwaomba Machinga hao watakaokuza mitaji yao na kuwa wafanyabiashara inawapasa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kwani kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Singida Bw. Apili Mbaruku alisema kuhusu vigezo vya kupata kitambulisho cha Machinga ni pamoja na Machinga kuwa na kipato chini ya milioni nne.

“Leo hii Mhe. Mkuu wa Mkoa utawapa vitambulisho Machinga 53 ambao wamekidhi vigezo ambapo kwa maelekezo tuliyopewa kila Machinga anawajibika kujaza fomu na kutia saini taarifa zake zilizo sahihi na endapo atatoa taarifa ya uongo mhusika atachukuliwa hatua stahiki”. Awali, Meneja Mbaruku alitilia mkazo.

Bw. Mbaruku aliongezea kuwa, vitambulisho hivi vitasaidia kuboresha biashara za wajasiriamali ili waweze kuwa walipa kodi wazuri nchini.

Naye Machinga anayefanya biashra ya kuchonga vitanda mtaa wa kambi ya fisi mjini hapa, Abdul Kachimba alisema amefarijika sana kupata kitambulisho cha Machinga ambacho atakitumia kufanya kazi ya biashara yake kwa ufanisi zaidi.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais wetu wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Magufuli ambaye ametupa fursa pekee sisi wajasiriamali kutusaidia vitambulisho hivi ambavyo vitasaidia kutambulika nchi nzima, hii ni chachu ya kutusaidia kwenda kwenye maendeleo ya biashara zetu ambapo hatimaye tunaweza kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao tutasaidia kuongeza pato la Taifa” alisema Kachimba.

Wafanyabishara wengine wadogo wa mkoa wa Singida wakipokea vitambulisho hivyo vya ujasirimali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa awamu ya Tano la kutambua na kuthamini kazi zinazofanywa na wafanyabiashara wadogo wenye mauzo ghafi chini ya milioni 4, wameshukuru kupatiwa vitambulisho hivyo ambavyo wamesema vitawaondolewa usumbufu katika ufanyaji wa biashara zao hapa nchini.

Zoezi hili limefanyika sanjari na utoaji mafunzo kwa wafanyabiashara 1000 wa Manispaa ya Singida kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania - MKURABITA ambayo yatawawezesha wafanyabiashara hao kutambulika rasmi na hivyo kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kupata mikopo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.