Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka wasimamizi wa mradi wa kilimo cha korosho cha pamoja kufunga akaunti zote za benki pamoja na kusimamisha upokeaji wa fedha kwa ajili ya ugawaji na usafishaji wa mashamba hayo mpaka watakapokamilisha zoezi la uhakiki kwa kulinganisha na fedha walizopokea na idadi ya mashamba.
Akiongea wakati wa kikao kilichohusisha kamati ya wilaya ya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa mkoa na wasimamizi wa mradi wa mashamba ya korosho kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni, Dkt. Mahenge amesema mradi huo umekuwa ukilalamikiwa na wadau wengi kwamba wamekuwa wakilipia fedha lakini hawajaoneshwa mashamba yao huku wengine wakidai kubadilishiwa mashamba na kutosafishiwa kama walivyolipia fedha zao.
Amesema tathimini hiyo iwasaidie kubaini kiasi cha fedha walizopokea na ukubwa wa mashamba waliyonayo ili busara zitumike kwa kufanya mawasiliano na wilaya za jirani ili kuweza kugawa mashamba mengine au kurudisha fedha.
Aidha RC. Mahenge akawataka viongozi hao kuandaa na kumkabidhi taarifa ya kuanzia mwaka 2017 itakayoonesha kiasi cha mashamba yaliyopimwa fedha zilizoingia na namna zilivyotumika kwa kila mwaka pamoja na changamoto zilizojitokeza ndani ya siku zisizozidi siku saba.
Hata hivyo amewataka viongozi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika na unatoa huduma kwa wananchi kama ilivyokuwa imepangwa
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza wakati wa kikao
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge akipitia taarifa ya mradi wa korosho
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika mkutano huo
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.