Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga leo Mei 26,2025 amefungua Rasmi zoezi la mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa za Anwani za Makazi katika Ukumbi wa VETA Singida kwa Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiwahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Dkt. Fatuma Mganga, amesema lengo la kuanzisha mfumo ni kuimarisha masuala ya utambuzi ndani na nje ya nchi na kuwezesha mazingira wezeshi ya kunufaika na fursa za uchumi wa kidigitali na kuleta maendeleo endelevu.
“Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alikuwa na dhumuni jingine kubwa la kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yetu na na nchi kwa ujumla na hili linawezekana kwasababu tutakapo tambua kila mmoja anaishi wapi ni nani na kila taasisi ipo wapi na anayeendesha taasisi ile moja kwa moja tunakuwa na usalama na ulinzi wa kutosha katika maeneo yetu,” amesema.
Dk.Mganga amesema kupitia operesheni ya anwani za makazi Mkoa wa Singida uliweza kusajili taarifa za anwani 351,324 sawa na asilimia 105.5 ya lengo la anwani 332,998 kwenye mfumo wa kidigitali wa anwani za makazi kwa wakati ule.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw.Elisa Mbize, ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema hayo leo katika hafla ya ufunguzi wa zoezi uhakiki wa taarifa za anwani za makazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Amesema zoezi la uhakiki wa taarifa za anwani za makazi ni miongoni mwa miradi ya kimkakati ambayo ambayo inalenga kujenga misingi madhubuti katika masuala ya utambuzi ili kuboresha utoaji na ufikishaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi ulifanyika nchi nzima 2022 kupitia Operesheni Anwani za Makazi iliyojenga kumuwezesha kila mwananchi kutambulika mahali anapoweza kufikishiwa huduma, operesheni hiyo iweka msingi wa kuanza kunufaika na fursa za uchumi wa kidigitali,” amesema Mbise.
Mbise mfumo huo pia ulilenga kuimarisha masuala ya kijamii ambapo jumla ya anwani za makazi milioni 12.3 zilisajiliwa kwenye mfumo wa kidigitali wa anwani za makazi unaojulikana kama NaPA ambapo dhamira ya wizara inakwenda sambamba na maelekezo ya serikali ya kuunganisha mifumo yote ya kutolea huduma.
Kadhalika,Amesema kuwa nchi yetu imeanza kunufaika na Mfumo wa Anwani za Makazi mfano Disemba 2023 kulipotokea janga la maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara makazi yaliyoathirika na maporomoko hayo yaliweza kutambulika kupitia mfumo huo.
Naye Mkurugenzi wa Fedha Idara ya Serikali za Mitaa, Mudrika Mujungu, ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amesema suala la usimamizi wa anwani za makazi ni jukumu la watendaji wa na wenyeviti wa serikali za mitaa hivyo kila mtu awajibike katika usimamizi wa mfumo huo.
"Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndio yenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazogusa wananchi tunalazimika kusimamia Mfumo wa Anwani za Makazi kwasababu ni mfumo unaokwenda kutoa huduma kwa wananchi" amesema Mujungu.
Katika mwaka 2022,Jumla ya vibao 331,341 vya namba za nyumba vilibandikwa pamoja na kusimikwa nguzo 6,953 za majina ya barabara ambapo katika Manispaa ya Singida jumla ya anwani za makazi 67,797 zilisajiliwa na vibao 49,322 vya namba za nyumba vilibandikwa na nguzo 1898 za majina ya barabara.
Wizara ya Mawasiliano na Teknolijia ya Habari imesajili na kutoa anwani mpya za makazi 535,856 kwenye halmashauri 40 ambazo zoezi la kuhuisha taarifa imefanyika kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi zenye tija kwa taifa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.