Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa bidii ili kupatikana tija itakayo saidia kuongeza mapato ambayo yataboresha maslahi ya Watumishi.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi lililofanyika Machi 9, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo ambapo alisistiza uwepo wa mahusiano mazuri baina ya watumishi ili kuongeza tija.
"Pia nipende kusisitizia kuwa bila tija Serikali haiwezi kupata mapato ambayo yataiwezesha kuboresha maslahi ya watumishi" alisema Serukamba
Aidha ameagiza Baraza hilo kutekeleza majukumu yake kuhusu taratibu zinazoweza kuchukuliwa ili kuleta ufanisi katika mifumo ya kutoa huduma kwa wananchi na kushauri mabadiliko ya kanuni za kudumu katika utumishi wa umma namna bora ya kuboresha mazingira. Serukama aliagiza wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha wanapitia rasimu ya bajeti kwa undani na kushauri kama kuna maeneo hayo yalisahaulika kabla havijafikishwa bungeni.
Hata hivyo RC Serukamba ameagiza Halmashauri zote Mkoani hapo ambazo mabaraza yake ya wafanyakazi yalimaliza muda wake kuhakikisha wanachagua mengine ili yaweze kuendelea kutetea maslahi ya watumishi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa Mwl. Dorothy Mwaluko amewaasa watumishi kutumia weledi katika kutekeleza majukumu ili kuleta tija iliyo kusudiwa huku akikumbusha kufuata mila na desturi za utumishi ili kufikia malengo.
"Utumishi una mila na desturi zake na mtumishi atapata tabu endapo atashindwa kuzifuata, tuishi maisha ya utumishi wa umma" Mwaluko
Aidha amehimiza watumishi kuwa wavumilivu na upendo katika kufanya kazi huku akibainisha kwamba hakuna mwenyekazi zake binafsi katika Mkoa hivyo watumishi wajifunze kushirikiana katika kutumia rasilimali zilizopo zikiwemo magari.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.