Bonanza lililowakutanisha waalimu kutoka Halmashauri mbili za Mkoa wa Singida,Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Singida lenye Jina la "Bonanza la Mwalimu na Samia"lililofanyika katika uwanja WA Bombadia mkoani Singida limefanyika mkoani Singida likiratibiwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Singida.
Katika Bonanza hilo Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,ametoa pongezi Kwa waalimu hao kama daraja imara kati yao na wanafunzi katika nyanja za masomo Kwa kuwajengea uwezo imara na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata ufaulu mzuri unaowawezesha kuendelea na masomo ya Sekondari na vyuo vikuu pamoja na msingi imara wa kujiajiri hata baada ya kumaliza masomo yao.
Amesema kuwa serikali inautambua mchango mkubwa WA waalimu na hivyo serikali itakuwa tayari wakati wote kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero zao ili kuendelea kuzitafutia ufumbuzi ili kuendelea kuwaunga mkono Kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi Kwa kujenga miundombinu Bora kuanzia shule ya awali na Sekondari na kuongeza vitendea kazi vya kutosha mashuleni.
"Waalimu wa Mkoa wa Singida mmeendelea kuwa baraka katika Mkoa huu kwani takwimu za ufaulu katika Mkoa wa Singida zinazidi kupanda juu tofauti na ilivyokua katika siku za nyuma kwani mnafanya kazi zenu Kwa weledi na uzalendo pamoja na changamoto zilizopo ambazo zitafanyiwa kazi"alisema Mhe.Dendego
Mkuu wa Wilaya ya Singida,Mhe.Godwin Gondwe akizungumza katika Bonanza hilo,amesema tuzo mbalimbali zinazotolewa Kwa waalimu ni kama motisha na zitasaidia kuongeza morali katika ufundishaji na kuwapongeza Kwa matokeo mazuri ikiwemo ya kidato Cha nne mwaka huu yaliyopanda ufaulu Kwa asilimia huku kukiwa na malengo ya kufuta daraja sifuri Kwa mwaka ujao wa 2025.
"Mpango wetu ni kuondoa daraja ziro kabisa mashuleni,hili litafanyika pia Kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vyakula mashuleni wote Kwa ujumla na sio Kwa madarasa ya mitihani pekee."alisema DC Gondwe
Naye mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu amesema serikali inaendelea kuunga mkono elimu Kwa kuhakiisha Kuna miundombinu Bora ya elimu kama kujenga mashule,madarasa ya kutosha,nyumba za waalimu,mabweni kufuta ada za wanafunzi kuanzia awali mpaka kidato Cha sita na kuongeza mikopo ya elimu ya juu ili kuwawezesha wanafunzi katika gharama za ada na kujikimu,Hivyo ni vema kuutambua mchango wa mwalimu kwa mkono mwalimu kwani ndie daraja la kuwezesha mafanikio ya wanafunzi.
"Ufaulu katika matokeo umeongezeka Kwa takribani asilimia Tano,hii ni kutokana na uboreshwaji WA mazingira ya kujifunzia na kufundishia Kwa waalimu na wanafunzi,ndio sababu ya mwitikio na hamasa kubwa inayoonekana Kwa waalimu kujitokeza Kwa wingi SIKU ya Leo kwasababu wana furaha kwani changamoto zao zinafanyiwa kazi."amesema Mstahiki Meya.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.