• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Dkt. Mahenge Atangaza Fursa kwa Wawekezaji Mkoani Singida

Posted on: May 14th, 2022

Wawekezaji wa aina mbalimbali wameaswa kuendelea kuwekeza Mkoani Singida kwa kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji na ni katikati ya nchi jambo ambalo linarahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Miundombinu ya Barabara  mazingira mazuri ya ki biashara yameendelea kuboreshwa Mkoani hapo ili kuvutia uwekezaji na biashara kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati akizindua ufunguzi wa duka jipya la vifaa vya Ujenzi lililopo Singida mjini  lijulikanalo kama NAJEL BUILDERS COMPANY LIMITED.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya Najel Builders LTD mkoani Singida

Dkt. Mahenge ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwaletea wana Singida huduma hiyo nakubainisha kwamba usambazaji wa bidhaa hizo za Ujenzi zitanufaisha mikoa yote ya pembezoni. 

Aidha ameitaka Kampuni hiyo kuuza vitu vyenye ubora wa Hali ya juu ili kuwanufaisha wananchi wa Singida lakini pia kuimarisha soko katika maeneo yote ya ndani na nje ya Mkoa.

Hata hivyo amewataka wawekezaji kuendelea kuwekeza kwa kuwa Serikali inaendelea kuboresha Mazingira ya Biashara ikiwemo kutenga maeneo mahsusi kwa wamachinga nakuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu amesema uwekezaji kama huo unafaida kwa Serikali na Manispaa kwa kuwa wanachangia kodi ya mapato ambayo itaharakisha maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya NAJEL BUILDERS Ltd Mhandisi Neema Nzwalile amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge kwa kukubali wito huo sambamba na mapokezi mazuri ya Serikali ya Mkoa huo katika sekta ya uwekezaji hali iliyoongeza chachu na hamasa kwa wawekezaji wazawa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo waheshimiwa Madiwani wa Singida Mjini, Wahandisi wa Ujenzi kutoka sekta binafsi, mafundi Ujenzi pamoja na wafanyabiashara wa mkoani Singida.


MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na wadau na washiriki mbalimbali katika sekta ya ujenzi, Wahandisi, Wafanyabiashara (hawapo pichani) waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa duka la vifaa vya ujenzi mkoani Singida 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Najel Builders L.T.D inayajihusisha na ujenzi na usimamizi wa miradi, usambazaji wa vifaa vya ujenzi Mhandisi Neema Nzwalile akimuonesha Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge baadhi ya bidhaa za ujenzi zinazopatikana katika duka hilo mara baada ya uzinduzi Mei 13, 2022

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Singida Mjini, Mkurugenzi wa Kampuni na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika uzinduzi huo.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.