Wizara ya mambo ya ndani imetakiwa kukamilisha kwa haraka mikakati ya ufungaji wa mifumo ya kamera za usalama katika majiji makubwa hapa nchini yakiwemo Dar es salaam Dodoma, Mbeya Tanga Arusha na Mwanza kwa kuwa mifumo hiyo itatumika kufuatilia mienendo ya watu ambao wenye nia ya kuvuruga amani na usalama katika maeneo hayo.
Pia Wizara hiyo imetakakiwa kuendelea kujenga miudombinu na makazi ya askari polisi na magereza ili kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi ambayo yanaongeza chachu katika kuimarisha ulinzi wa Raia na mali zao.
Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 30.08.2021 wakati wa ziara yake mkoani Singida ambapo alizindua majengo mawili ya ofisi za Kamanda wa Polisi na ofisi ya mkuu wa Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani humo.
Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu amempongeza IGP Sirro kwa usimamizi mzuri wa majengo hayo ambapo Jengo la ofisi ya Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia limegharimu kiasi cha milioni 499 na jengo la mkuu wa polisi mkoa wa Singida limegharimu shilingi 469.4
Aidha katika ziara hiyo Waziri Mkuu amelitaka Jeshi la Polisi nchin kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassani kusimamia haki na kuhakikisha wanapunguza matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa Raia.
Hata hivyo Waziri Mkuu amelitaka Jeshi hilo kutumia wasanii na vipeperushi kwa kupeleka elimu kwa jamii ili kuwashirikisha katika masuala ya ulizi na usalama pamoja na kuimarisha madawati ya jinsia kwa kila eneo ili kupunguza dhana za uhalifu katika jamii.
Aidha Waziri Mkuu amewataka kushirikisha vyombo mbalimbali vya sheria ili kusaidia kupunguza mlundikano wa kesi na mahabusu hapa nchini.
Kwa upande wake IGP SIRO amesema Ujenzi wa majengo haya mawili umekamilishwa tarehe 15/07/2021 kwa gharama ya Tshs 1,314,299,300. kwa majengo yote mawili.
Jengo la ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia likiwa na jumla ya vyumba vya ofisi 14 na linatosheleza mahitaji.
Aidha jeshi la polisi limejiwekea mkakati wa kutoa elimu kwa wananchi kuliamini Jeshi lao na kuwafichua Wahalifu na Uhalifu pamoja na kushirikiana kwa karibu na wananchi, viongozi wetu wa Vitongoji, Vijiji, Mitaa, Kata, Tarafa, Wakurugenzi, Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya, Mikoa hadi Taifa katika kutekeleza mikakati ya ulinzi na usalama kwenye maeneo yetu.
IGP Sirro amesema tayari watekeleza mpango wao wa Kupunguza mlundikano wa Mahabusu kwenye vituo vya Polisi na Mahabusu Magerezani kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya Sheria hususani Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali – DPP na Jeshi la Magereza.
Aidha IGP amemhakikishia waziri mkuu kwamba Jeshi la Polisi mkoani Singida litaendelea kujenga na kuboresha miundo mbinu ya majengo ya Jeshi la Polisi nchini hatua kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha kwa lengo la kuwajengea mazingira mazuri ya kazi Maafisa, Wakaguzi, Askari na Watumishi Raia.
Awali RC Singida Dkt. Binelith Mahenge amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara, madaraja, ujenzi wa shule na umeme ambapo kila wilaya kuna miradi mbalimbali inaendelea
Amesema katika wilaya ya Mkalama kuna mradi wa ujenzi wa madarasa unaendelea lakini kuna ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya, daraja linalounganisha mkoa wa Simiyu na Singida .
Hata hivyo RC ameeleza uwepo wa changamoto ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi na kumuomba Waziri mkuu aweze kuona namna ya kusaidia kwenye utatuzi wa changamoto hiyo.
Mwisho
Imeandaliwa na
Ofisi ya RC- Singida .
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.