Zaidi ya Hati 700 zimetolewa katika hafla ya ugawaji wa Hatimiliki za kimila kwa wananchi wa Ikungi mkoani Singida kupitia mradi wa pamoja wa Kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi JP-RWEE huku asilimia 40 za hati hizo ni hati za wanawake na wasichana.
Hayo yamefanyika hii leo tarehe 10 Januari, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo Waziri wa Ardhi, Nyuumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki katika tukio hilo.
Akizungumzia mradi huo amesema kuwa ni matokeo ya mradi wa awali ambapo utekelezaji wake unafanyika tangu mwaka 2023 hadi ifikapo mwaka 2027 ukitekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na wadau kama vile FAO, WFP, UN WOMEN, IFALD chini ya ufadhili wa Sweden na Norway.
Akizungumzia suala la migogoro ya ardhi,Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mhe. Thomas Apson amesema kuwa sababu kubwa inayowakabili wananchi wa Wilaya ya Ikungi ni uelewa mdogo wa sheria ya ardhi hivyo kupelekea ongezeko la migogoro ya ardhi wilayani hapo.
“Ugawaji wa hati miliki za kimila unaofanyika hii leo ni suluhisho la migogoro hio .Tunaishukuru sana Wizara kwa kuweka miundombinu rafiki kutokana na mipango ya ardhi” amesema Mhe.Apson.
Akisoma taarifa katika gafla hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ameainisha baadhi ya vijiji 12 vinavyonufaika na mradi huo ikiwa ni pamoja na Kipumbwiko, Wibia, Puma, Samaka, Matongo na vinginevyo.
Baadhi ya wananchi wanaonufaika na tukio hilo, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jamboi hilo ambao ni mkombozi kwa na litasaidia kuepusha migogoro mbali mbali na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji kwa amani.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.