Maafisa masuuli katika Wilaya ya Ikungi wameelekezwa kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa ununuzi wa umma NeST katika michakato yote ya ununuzi wa umma.
Hayo yamesemwa leo (Januari 13, 2025 )na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Kijazi alipozungumza katika mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi.
Mkurugenzi ameongeza na kusema kuwa watumishi wote wanaohusika na mchakato wa ununuzi ndani ya Taasisi wanapaswa kupata mafunzo yatakayowawezesha kutumia mfumo huo wa manunuzi kwa ufasaha ili kuepusha ubadhilifu wa fedha za Serikali.
"Wanaopaswa kushiriki mafunzo hayo ni pamoja na maafisa masuuli, Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa wawili kwa kila idara au kitengo wanaohusika na manunuzi, Mkaguzi wa ndani, Maafisa Tehama na Mwanasheria wa taasisi." amezungumza Kijazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya manunuzi Wilaya ya Ikungi Bi Mariam A. Haroun amesema kwa mujibu wa kifungu Cha 9 (1)(k) cha sheria ya ununuzi wa umma, sura ya 410, mamlaka ya kudhibiti wa ununuzi wa umma( PPRA )imekasimiwa jukumu la kusanifu, kuanzisha na kuhuisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya uwazi na kuleta tija kwenye ununuzi wa umma.
"Ni wajibu wa kila mmoja wetu kujifunza mfumo wa NeST na kujisajili ili kurahisisha huduma za manunuzi kwa njia ya mtandao" amesema Bi.Mariam
Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya watumishi waliopata mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yanaenda kuwa suluhu dhidi ya upotevu wa fedha za Serikali kwani manunuzi yote yanaenda kufanyika kwa njia ya mtandao( NeST )na wapo tayari kujisajili na kuanza kutumia mfumo huu rasmi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.