• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Iramba kukabidhi vyumba vya madarasa 61 kabla ya Desemba 5, 2021

Posted on: November 30th, 2021

Wilaya ya Iramba mkoani Singida inatarajia kukabidhi jumla ya vyumba vya madarasa 61 ambavyo ni miradi ya elimu  yenye thamani ya Sh. Bilioni 1.89 iliyojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO 19  ifikapo tarehe Desemba 5, 2021.

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 30, 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Michael Matomora  alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kyengege Kata ya Kyengege.

Aidha amebainisha kwamba miradi yote imefikia hatua ya kupauliwa na tayari wasafirishaji wapo Dar es Salaam kuchukua mabati ambapo tunatarajia ndani ya siku mbili au tatu yatakuwa yamefika katika maeneo ya kazi, hivyo ni imani yetu kwamba mpaka tarehe tano tutakuwa tumemaliza kupaua kwa sababu tumesha nunua kila kitu, Alisema Matomora.

Mkurungezi huyo akabainisha kwamba katika miradi hiyo 47 ni ya ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari 19 ambazo zitagharimu kiasi cha sh.Milioni 940

Aidha Mkurugenzi huyo akaeleza kwamba miradi 14   ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 14 katika shule shikizi  saba (7)  ambazo ni Ulongo, Magugu, Kagera, Itunda, Masunkune, Kisingu na Ibambasi ambazo zitagharimu kiasi cha Tsh. Milioni 280.

Amesema kwa ujumla Shule ambazo zinatekeleza miradi ya UVIKO 19 katika wilaya ya Iramba ni Lulumba, New Kiomboi, Kinambeu, Shelui, Kyengege, Kizaga, Kidaru, Mbelekese na Mtekente. Nyingine ni Mtoa, Tulya, Ntwike, Urughu, Ushora, Kinampanda, Mukulu, Mgongo, Kaselya na Kisiriri. alifafanua Matomora.

Akijibu baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo baadhi ya wakuu wa Shule kutotizimiza majukumu yao vizuri Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote wa Serikali atakaye sababisha uzembe katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Yeyote atakayefanya uzembe wa makusudi tutamchukulia hatua za kinidhamu ili iwe fundisho kwakwe na wengine wenye tabia kama hizo, lengo likiwa sio kumkomoa bali ni kwa ajili ya manufaa ya jamii husika. Alisema Dkt. Mahenge.

Hata hivo RC Mahenge amewapongeza  viongozi  wa wilaya ya Iramba kwa jitihada zao katika kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo ambapo mpaka sasa madarasa yote yamefikia hatua ya  kupaliwa.

Aidha RC. Mahenge akawataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba pamoja na viongozi wa CCM kuendelea kusimamia kazi hizo na kuhakikisha kwamba inakamilika kabla au ndani ya Desemba 5, 2021.

Awali Suleiman Mwenda akimkaribisha Mkuu wa mkoa alisema wilaya inatekeleza miradi 47 ya ujenzi wa madarasa  katika shule 19 ambapo jumla ya madarasa 18 yamefikia hatua kupauliwa  katika shule saba (7)

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.