• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Itigi Wafikia Pazuri Anwuani Za Makazi

Posted on: April 20th, 2022

Halmashauri ya Itigi mkoani Singida imefikia asilimia 88 za anwuani za makazi kwa kuyafikia majengo 30,789 kati ya  35,000 yaliyokuwa yametarajiwa pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa kazi hiyo.

Akitoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo John Mgalula amesema  taarifa za makazi  zimekusanywa katika Kata 13 za Halmashauri hiyo na kazi ya ukusanyaji na uingizaji wa taarifa  katika mfumo unaendelea kwa maeneo yaliyobaki.

Amesema taarifa zilizobaki wanategemea zitakamilika kwa ukamilifu wake ifikapo mwishoni mwa wiki hii ambapo zoezi litakaloendelea litakuwa la kupachika vibao katika mitaa mbalimbali huku vingine vikiendelea kutengenezwa.

Akizitaja baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo Mgalula amesema Upungufu wa fedha za utekelezaji wa zoezi hilo pamoja na umbali wa baadhi ya maeneo pamoja na ukosefu wa mitandao ya simu katika baadhi ya vijiji jambo ambalo limesababisha kupungua kwa kasi ya utekelezaji wa zoezi husika.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema Halmashauri imeendelea kukusanya fedha kupitia vyazo mbalimbali vya mapato ili kutatua baadhi ya changamoto zilizojitokeza.

 

Pamoja na hayo Mkurugenzi akaendelea kuomba ngazi ya Mkoa huo pamoja na Wizara kuangalia changamoto za mfumo ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara ambazo zimechangia kutofikiwa malengo kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge akijibu hotuba ya Mkurugenzi amewapongeza kwa hatua waliyoifikia na kuwataka kuhakikisha wanafikia lengo ifikapo mwisho wa wiki hii ili kuwezesha kukamilika kwa zoezi na kuandaa taarifa ya pamoja ya Mkoa.

Aidha, ameagiza Halmashauri hiyo kufanya mawasiliano ya karibu na chuo cha VETA wilayani hapo ili kupata vibao vya barabarani kwa gharama nafuu huku akiagiza kushirikishwa Idara na taasisi mbalimbali katika upatikanaji wa vibao hivyo.

Awali RC alikagua Mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Kitaraka ambapo amewapongeza wananchi wa Kata hiyo ambao wamejitolea nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo na kuahidi kwamba atahakikisha kwamba Ruwasa na Tanesco wanafikisha huduma ya maji na umeme kabla ya wanafunzi kuanza masomo.

Mradi huo unahusisha  jengo la Utawala lenye thamani Tsh. Milioni 82.8, madarasa manne yenye thamani ya Tsh.Milioni 253.16, Maabara ya kompiuta yenye thamani ya milioni 32.92, Maktaba yenye thamani ya Milioni 56.5,  vyumba vitatu vya Maabara vyenye thamani ya Tsh. Milioni 208, matundu 20 ya vyoo yenye thamani ya Milioni 46.8 pamoja na ujenzi wa tanki la maji.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa shule ya Sekondari Itigi Mwl. Jacob Mwabeza imebainisha  kwamba ujenzi huo mpaka kumalizika utagharimu kiasi cha Tsh. Million 680.2 na mradi unategemewa kukamilika kabla ya tarehe 28 Mei 2022.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.