• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

JAFFO AAGIZA HALMASHAURI NCHINI KUIGA UFANISI WA MIRADI IKUNGI

Posted on: December 10th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo amempongeza hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bw. Justice Kijazi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya eneo hilo kwa gharama ndogo sana ikilinganishwa na uhalisia.

Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kupitia mfumo wa ‘force account’, wameweza kutumia kiasi cha sh. 420 milioni pekee kujenga ukumbi wa mikutano wa kisasa na wenye viwango, na 200 kujenga jengo kubwa la ofisi, huku akisisitiza kwa kuzitaka halmashauri ambazo bado hazijaanza ujenzi wa majengo ya ofisi na kumbi za kisasa za mikutano kuja kujifunza Ikungi.

Waziri Jaffo akiwa kwenye ziara ya kawaida mkoani Singida, na kupata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, na miradi mingine ya halamshauri akitokea Jijini Mwanza, alisema katika uongozi wake amepita kwenye halmashauri nyingi lakini hajawahi kukutana na jengo la ukumbi mzuri na wa kisasa kama huo wa halmahauri ya Ikungi.

“Mkurugenzi kilichonifurahisha ni namna mlivyozingatia thamani ya pesa(value for money) na ubora, nilisema nataka ofisi ya TAMISEMI ifanye mabadiliko na mapinduzi ya kiutendaji, tulikotoka huko nyuma hatukuwa na sifa nzuri, lakini leo hii kila mahali ukitazama ikiwemo hapa ikungi huwezi kuamini,” alisema

Alizitaka halmashauri za Kondoa na Iramba kwa kuanzia kuja kujifunza kupitia wenzao hao wa Ikungi, ambao idadi ya majengo yao yote yamegharimu sh 1.5 bilioni pekee “nataka wengine wakitaka kujenga ofisi waje kujifunza hapa, iwe duplicate kwa wengine kuja kucopy na kupaste,” alisema Jaffo

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema kiasi hicho cha pesa sh 1.5 bilioni kilitolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa halmashauri hiyo kwenye eneo la utawala bora.

Alisema kati ya pesa hizo sh 1.3 milioni zimetumika kujenga ofisi, nyumba ya DC, na Hospitali ya wilaya, huku Serikali ikiwa tayari imewatengea fedha nyingine zaidi ya sh. milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa vituo vya afya vya Sepuka, Ihanji na Iyumbu.

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi, alisema tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2013, watumishi wa eneo hilo wamekuwa wakipanga na kukodi majengo ya watu binafsi kwa mikutano mbalimbali, ikiwemo kutumia hadi nyumba za wageni kwa shughuli za ofisi.

Kijazi alisisitiza kuwa jengo la ukumbi huo mpya na wa kisasa mbali ya kutumika kwa shughuli mbalimbali za mikutano ya kikazi, lakini pia litatumika kama kitega uchumi cha kuingizia halmashauri hiyo mapato, huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Ali Mwangi, akimuomba Waziri Jaffo kusaidia mchakato wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya kwa ustawi wa afya ya wakazi wa eneo hilo.

Hata hivyo, pamoja na kufurahishwa na Ikungi lakini hakufurahishwa na utendaji na usimamizi wa miradi ya vituo 2 vya afya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Iramba (Ndago na Kinampanda), ambavyo kwa mda mrefu ujenzi wake umekuwa ni wa kusuasua.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo akizungumza na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali muda mfupi mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa ajili ya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi iliyopo katika Manispaa ya Singida na Ikungi mkoani Singida.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo (watatu kutoka kulia) muda mfupi mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya cha Sokoine katika halmashauri ya Manispaa ya Singida ambapo amelidhishwa na huduma, usimamizi na utendaji kazi unaoendelea kutolewa kwa wagonjwa katika kituo cha afya cha Sokoine Manispaa ya Singida.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo (kushoto) akizungumza na Mtaalamu wa Maabara Bi. happyness Nyaruke katika kituo cha afya Sokoine 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi kabla ya kuanza ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo mkoani Singida.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo (wapili kutoka kushoto) akipokea ufafanuzi zaidi juu ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi Hagai Mziray wa kampuni ya Mzinga Holding (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo mkoani Singida.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo (katikati) akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Bw. Justice Kijazi (kushoto) juu ya ujenzi wa ofisi na ukumbi wa halmashauri hiyo.



MUONEKANO WA BAADHI YA MAJENGO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe. Juma Ali Mwangi akizungumza 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.


Mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw. Edward Mpogolo akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo, akizungumza na watumishi  wa halmashauri hiyo wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.

KIKAO KIKIENDELEA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.