Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoa Singida limeundwa rasmi likienda sambamba na uchaguzi wa viongozi mbalimbali ambao watawakilisha Mkoa huo katika ngazi ya Taifa.
Akiongea baada ya Mkutano huo Mratibu wa Jukwaa hilo ngazi ya Mkoa Jonathan Semiti amesema kwamba kazi kubwa iliyofanyika ni kuunda jukwaa na kuchagua viongozi watano huku wakiwapitisha katika muongozo wa namna ya kuendesha majukwaa hayo.
Semiti amesema lengo la Serikali kuanzisha jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ni kuhakikisha wanajikomboa kiuchumi kwa kuwajengea uwezo na kuwakutanisha wanawake ili waweze kujadili fursa za kiuchumi na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi nchini.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Shukrani Mbago amesema jukwaa hilo ni muhimu katika kuwezesha wanawake kwenye masuala ya biashara na uchumi kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo wanayoishi.
Naye Katibu wa jukwaa Priscadiana Maleta amefafanua kwamba wao kama viongozi watahakikisha wanafikia wanawake wote Mkoani hapo kupitia majukwaa ya kata na vijiji ili kuwasaidia kuziona na kuzifikia fursa zilizopo Serikalini na sehemu nyingine.
Naye Mwenyekiti wa jukwaa hilo Zamda Ahamedi John amebainisha kwamba jukwaa litawasaidia kuwafikia wanawake wote Mkoani hapo na kujua changamoto zinazowakabili na kujua mahitaji yao katika kujikwamua.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.