Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amewataka wananchi kote nchini waasithubutu kuchagua wagombea watakaotoa rushwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani kufanya hivyo watachagua viongozi wabovu ambao hawataharakisha maendeleo kwenye maeneo yao.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge ametoa kauli hiyo kwenye viwanja vya bombadia mjini Singida wakati anazungumza mara mamia ya wananchi waliojitokeza baada ya risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mnzava amewasisitiza wananchi kuchagua Viongozi wenye sera na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo na sio viongozi wanatoa rushwa kwa sababu wakichaguliwa wataangalia maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya wananchi.
"Msiwachague Viongozi wanaotoa rushwa watawarudisha nyumba kwa sababu hatawaletea maendeleo bali watajijali wao tu," Ameeeleza Mnzava.
Akizungumza na Vijana zaidi ya 1000 kwenye Kongamano la Vijana mjini Singida, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge Uhuru Godfrey Mnzava amewahimiza Vijana kuwa wazalendo katika Taifa lao na wadumishe amani na utulivu katika nchi yao.
Amewaomba vijana wenye sifa na uwezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu anaamini kuwa wanauwezo wa kufanya vizuri pindi watakapochaguliwa.
Baadhi ya Vijana walioshiriki kwenye Kongamano hilo wameiomba Serikali kuitisha mikutano na makongamano kama hayo kwa sababu yatawasaidia kufahamu fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo nchini pamoja kuwaimarisha kimaadili na kiuzalendo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.