Wakazi wa Mkoa wa Singida wametakiwa kujenga tabia ya kuyatembelea maeneo ya historia na kijifunza histrioa ya mkoa wao na nchi yao kwa ujumla ili waweze kutambua walivyokuwa wakiishi watu wa maeneo hayo kabala na baada ya uhuru.
Imebainika kwamba ili kujua hatua ambazo nchi imeweza kupiga na kuleta maendeleo ya uchumi, siasa na utamaduni ni lazima kuijua historia ya zamani ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo Desemba 5, 2021 na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya kihistoria yakiwemo Ofisi ya DC wa kwanza Muafrika iliyopo Manyoni Mkoani Singida, Nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Mjini Kati Manyoni, vituo mbalimbli vya kihistoria eneo la Kilimatinde na reli ya mwendo kasi iliyopo Makutopora ambapo alibanisha umuhimu wa kujifunza historia ya maeneo hayo.
Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru ambayo Mkoa wa Singida unaendelea kuadhimisha kwa namna tofauti mpaka itakapofika Desemba 8 mwaka huu kabla ya kuungana na maadhimisho ya ki taifa yatakayofanyika tarehe 9 katika uwanja wa uhuru mkoani Dar es salaam.
Mwaluko akafafanua kwamba pamoja na historia lakini wananchi wa Mkoa wa Singida wanapashwa kufahamu jitihada za Serikali katika kuliletea taifa maendeleo kwa kuanzisha reli ya mwendo kasi ambayo imesemekana itarahisisha usafiri na kuongeza biashara maeneo mbalimbali.
Ziara hiyo ilihusisha wakurungezi wa Halmashauri saba za Mkoa wa Singida, Wakuu wa Wilaya ya Singida Mjini na Iramba pamoja na wabunge mbalimbali lengo likiwa ni kuwaonesha wananchi fursa nyingine za ki utalii ambazo huweza kulisaidia taifa kupata mapato kupitia vitu vya kihistoria.
Naye DC wa Singida Mjini Mhandisi Pasikas Muragili akimwakilisha DC wa Manyoni akatumia muda huo kuwataka Vijana kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kuwa yana mafunzo ndani yake.
DC Muragili akawataka pia vijina kujitokeza siku ya tarehe sita katika ukumbi wa mikutano wa Halamashauri ya wialaya ya Manyoni kushiriki kongamano juu ya hatua mbalimbali zilizofikiwa na Serikali kabala na baadaye.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.