• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Maadhisho ya miaka 60 ya Uhuru mkoani Singida vijana wafanya Kongamano

Posted on: December 6th, 2021

Vijana wametakiwa kuenzi miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara na miaka 59 ya Jamhuri kwa kuangalia  mabadiliko katika nyanja za uchumi utamaduni na namna ya upatikanaji wa viongozi unavyofanyika hapa nchini.

Mkuu wa ya Iramba Suleimani Mwenda akihutubia wakati wa kongamano la vijana katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kimkoa ya miaka 60 ya uhuru wa Tanznaia Bara.

Akiongea katika kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,  Mkuu wa ya Iramba Suleimani Mwenda amesema hali ya uchumi wa taifa umebadilika kwa kiasi kikubwa kabla na baada ya uhuru hivyo vijana wanatakiwa kujifunza kutokana na mabadiliko hayo.

DC  Suleimani akabainisha kwamba katika kipindi cha baada ya uhuru kulikuwa na chuo Kikuu kimoja  cha Dar es Salaam ambacho kilichukua wanafunzi wachache hivyo kusababisha waliowengi kukosa fursa ya kupata elimu ya juu, ikilinganishwa na kipindi hiki ambapo vyuo ni vingi.

Amesema ukizungumzia uhuru wa Tanzania unazungumzia uhuru wa nchi nyingi za kiafrika kwakuwa Tanzania ilishiriki katika kutafuta ukombozi wa mataifa mengi ya kiafrika  yakiwemo  Msumbiji, Afrika ya Kusini jambo ambalo vijana wanatakiwa kufahamu hali ya ukarimu ambao umekuwa ni sehemu ya utamaduni wetu. 

Aidha siasa za Tanzania hasa namna ambavyo viongozi wamekuwa wakibadilishwa kwa njia ya chaguzi ambapo mataifa mengi yamekuwa yakishikwa na butwaa hasa kwa kuangalia nchi za jirani na Tanzania ambazo zimekuwa zikiingia kwenye migongano mara kwa mara.

Awali DC huyo alitoa shukrani za dhati kwa wandaaji wa kongamano hilo ambalo linawafungua vijana na kuwafanya kuwa wazalendo na kuwaonesha fursa mbalimbali zinazowazunguka.

DC Mwenda akabainisha umuhimu wa kufanyika kongamano hilo wilayani Manyoni kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya  kuwafundisha vijana umuhimu wa Mashujaa waliotokea Manyoni katika mapambano ya kudai uhuru.

Afisa Vijana Mkoa wa Singida Fredrick Ndahani akizungumza wakati wa kongamano hilo

Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida Fredrick Ndahani akaishukuru Serikali kwa kufufua na kuendeleza shirika la ndege nchini na ambapo  awali lilikuwa na ndege moja  lakini  baada ya miak 60 ya uhuru shirika lina ndege 11.

Ndahani alisema shirika hilo linatoa fursa kwa vijana kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwa kwa kuwa miundombinu ya barabara  na anga vimeendelezwa kwa kiasi kizuri.

Bwana Ndahani akafafanua kwamba ni jukumu la vijana kulinda miundombinu ya barabara na reli kwa kuwa ndio vitu ambavyo vitawakomboa vijina katika mpango wa usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.

Afisa Vijana huyo akamalizia kwa kusema kwamba mkoa wa Singida unajivunia kuwa na shule nyingi za Sekondari na Msingi ambapo hakuna kijana ambaye ataweza kufaulu akakosa shule alifafanua Ndahani.

Kongamano hilo lilihusisha vijana wajasiriamali, wanafunzi wa shule mbalimbali za wilayani hapo, Maafisa wa Serikali pamoja na umoja wa vijana wa chama cha Mapindizi CCM.

MATUKIO KATIKA PICHA

Vijana wakifuatilia kongamano hilo

Elimu ya Afya ikitolewa wakati wa kongamano hilo


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.